1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MASHARIKI YA KATI:

9 Februari 2005

Matokeo ya mkutano wa kilele kati ya waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon na rais wa Mamlaka ya ndani ya wapalestina Mahmoud Abbas ndio mada kuu iliogonga vichwa vya habari katika safu za maoni za wahariri wa Ujerumani.Maoni jumla ya wachambuzi ni kuwa maafikiano ya wanasiasa hao 2 kuweka silaha chini ingawa yanatoa matumaini ya amani katika Mashariki ya kati,shaka shaka lakini zimesalia.

Likichukua msimamo huo, gazeti la VOLKSZEITUNG linalochapishwa mjini Leipzig laandika:

".............Abbas anapaswa kufikia mapatano na chama cha HAMAS kiweke silaha chini iwapo anataka kukubalika kimataifa.Sehemu kubwa ya wapalestina wanaamini juu ya hivyo, kuwa waziri mkuu Sharon bila mtutu wa bunduki asingekua tayari kuuhama mwambao wa Gaza.Endapo Mahmoud Abbas akishindwa kuyatumia mapatano haya ya kusitisha mapiganio kuvuna matunda ya kisiasa,basi lini litazuka shambulio jengine la kigaidi kuchafua hali hii mpya iliozuka, ni swali la wakati tu.Na hapo jibu gani atalitoa Sharon likizuka shambulio hilo huhitaji kuagua."-Hilo lilikua Frankfurter Rundschau.

Ama gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU halkadhalika lina shaka shaka likiandika kuwa hata katika mkutano wao wa kwanza kabisa Bw.Sharon na Bw.Abbas ,yafaa kuwa na wasi wasi iwapo mkutano huu wa waisraeli na wapalestina unafungua kweli mlango wa matumaini.hatahivyo, ni hatua ya kihistoria kwa wanasiasa hawa wawili kukutana kwa mara ya kwanza na kujitwika jukumu la kusimamisha mapigano na kunyemeleana.....hilo lilikua Frankfurter Rundschau.

"Bado mapatano ya kuacha mapigano si chochote si lolote zaidi ya kuwa ni kutia nia tu-laandika gazeti la MÄRKISCHEN ALLGEMEINE kutoka Potsdam. gazeti linaongeza kuandika kuwa, mtihani unaokabili maafikiano hayo utakuja pale litakapozuka shambulio la kigaidi na hapo tena itaobainika Mahmoud Abbas na Ariel Sharon kwa kadiri gani wamepania kuziba mwanya wa tofauti kati ya wapalestina na waisraeli.

Ufunguo wa kuleta amani katika eneo hili upo katika ufumbuzi alioutoa baba wa rais wa sasa wa Marekani-yaani -kubadilishana ardhi kwa amani.

Gazeti la DIE WELT kinyume na magazeti hayo mengine linanin’giniza matumaini kutoka kikao cha jana huko Sharm el Sheikh.Laandika,

"Katika mashariki ya kati amani yamkinika.Kuliko ilivyokuawakati wowote kabla, kuna fursa za maskizano baina ya Israel na wapalestina,ingawa kila upande utabidi ujitoe mhanga katika madai yao.Hii inahitaji uongozi ,imani na usalama-bidhaa adimu wakati huu huko mashariki ya kati.

Hatahivyo, hali ya mambo haikuwahi kuleta tamaa kama sasa."

Ama gazeti la NEUE WESTFÄLISCHE kutoka Bielefeld laandika:

"Muhimu kabisa itakayoamua ni msimamo wa Marekani na kwa kadiri fulani wa Umoja wa Ulaya.Bila msaada na shinikizo kutoka nje itakua vigumu kurejea katika mazungumzo ya amani.Kwani,wajumnbe wote ha wa wili wana matatizo yao binafsi na ya kutosha miongoni mwa wananchi wao.Sharon anakumbana na changamoto na walowezi 250.000 wakati Abbas na vikundi vya wanamgambo wa kipalestina."

Katika mashariki ya kati yafaa tena sasa kuota ndoto ya amani.tangu jana matarajio yamechomoza tena kufuatia mkutano wa kilele wa Mashariki ya kati.Kipindi cha baridi yabisi cha diplomasia kimekiukwa na hatua za kujenga imani kati ya pande zote mbili zimeafikiwa.Lakini hata mradi huu wa kuleta amani ukishangiriwa namna gani,waweza ukatiwa munda na shambulio moja la kigaidi.Na hapo ndipo dalili hizi za sasa za amani zitaanza tena kutoweka.Kwahivyo, kuna dalili ndogo tu za kufungua mlango wa amani."

Likitumalizia uchambuzi huu, gazeti la OSTSEE-ZEITUNG laandika:

"Matumaini yanatupa mazungumzo yalioanzishwa upya tangu wiki sasa ambayo kilele chake tutumai hakitakua kikao cha Sharm el Sheikh.Lakini kunahitajika bado ufumbuzi wa maswali magumu kati ya waisraeli na wapalestina-swali la wakimbizi wa kipalestina,hadhi za jiji la Jeruselem,ujenzi wa maskani za walowezi wa kiyahudi na kuchorwa kwa mipaka kati ya pande hizo mbili.Wakati huu bado si mada za kujadiliwa.

Lakini, ni mada hizi zitakazoamua mwishoe, kwa umbali gani kila upande uko tayari kumridhia mwenziwe na iwapo wafuasi wenye siasa kali kila upande wataweza kudhibitiwa.Sharm el Sheikh,kwa kila hali maana yake ni kumaliza hali ya muda mrefu ya kukwama kwa juhudi za amani."

Kwa maoni hayo,kutoka OSTSEE-ZEITUNG ndio sina budi kuishia hapo kutoka gazetini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW