1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Masheikh wa Uamsho waachiliwa huru

Salma Said16 Juni 2021

Masheikh wawili wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) waliokuwa wanashikiliwa kwa miaka tisa sasa katika magereza ya Ukonga Dar es Salaam hatimaye wameachiwa huru.

Sansibar SHEIKH FARID HADI AHMED
Picha: Salma Said/DW

Mashehe hao waliachiwa huru JUmanne jioni baada ya kesi yao kukamilishwa kwa njia ya kiteknolojia huku wakipewa masharti makubwa katika kuachiwa kwao.

Taarifa za kuachiwa Masheikh hao wawili kati ya 51 zimeanza kusambaa majira ya saa 11 Alfajiri baada ya kiongozi wa Masheikh hao Sheikh Farid Hadi Ahmed kuonekana akiongoza sala ya Alfajiri katika msikitini eneo la Beit Al Raas mjini Unguja jambo ambalo liliwashangaza wananchi wetu.

SHEIKH MSELLEM ALI MSELLEMPicha: Salma Said/DW

Soma pia: Viongozi wa Uamsho wafikishwa Mahakamani Zanzibar

Baadhi ya taarifa kwenye mitandao zilipoanza kusambaa niliwatafuta walipo kila mmoja alipelekwa katika eneo lake ambalo sio la kawaida.

Majira ya saa 10 baada ya kumaliza kesi walipelekwa uwanja wa ndege kwa ajili ya kufikishwa Zanzibar.

Abdallah Juma ambaye ni miongoni mwa mawakili tisa wa masheikh hao amesema yeye na mawakili wenzake wote hawana taarifa ya kusikilizwa kwa kesi dhidi yao ila wanashukuru kuwa wameshatolewa.

Hivi juzi Mkurugenzi wa Mashtaka Sylvester Mwakitalu aliwatembelea na kuwahoji masheikh hao.

Uchambuzi kuhusu kuachiwa mashehe wa Uamsho

This browser does not support the audio element.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW