1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MASHINDANO YA RIADHA YA DUNIA YAMALIZIKA HELSINKI-ETHIOPIA YAWIKA

15 Agosti 2005

Mashindano ya riadha ya ubingwa wa dunia yalimalizika rasmi jana mjini Helsinki,Finland . Marekani ikiongoza orodha ya medali za dhahabu. Ethiopia upande wa Afrika ilifanya uzuri sana.

Kenya ambayo nusra iondoke mikono mitupu bila medali ya dhahabu, ilinyakua jana medali hiyo katika masafa ya mita 5000 ambamo Benjamin Limo alitoka nyuma na kuzima vishindo vya Muethiopia Sileshi Sihine.Kwa muda wa dakika 13:32.55,Limo aliifutia Kenya aibu katika mashindano haya kwa kutwaa medali ya dhahabu.Mbio hizi zilipokaribia kumalizika,Sihine alishika uongozi katika jaribio lake la kuwanyima kabisa wakenya medali ya dhahabu,lakini limo aliwaambia waethiopia mara hii kutangulia si kufika.

Sishine amejipatia hapo medali yake ya pili ya fedha kutoka mashindano haya ya Helsiniki,kwani alikwisha chukua medali ya fedha katika mita 10.000 alipomfuata Kenenisa Bekele kushinda mbio hizo.

Kenya ilipata medali ya fedha katika mbio za marathon wanawake ambamo muingereza Paula Radcliffe mara hii alitamba. Ndereba wa Kenya alibidi kuridhika na medali ya fedha.Tanzania pia ilitamba upande wa wanaume katika mbio za marathon na kurudi nyumbani na medali ya fedha.

Wasichana wa Urusi walishinda mbio za mita 400X4 kupokezana wakiwaachia wale wa jamaica medali ya fedha na wale wa uingereza wakichukua shaba.

Kwa upande wa wanaume, timu ya Marekani ya masafa hayo ya mita 400X4 ilitamba na kutoroka na medali ya dhahabu.

Katika kurusha mkuki, msichana wa Cuba alivunja rekodi yake binafsi ya dunia kwa centimita 16 na kunyakua taji la dunia.Bingwa wa olimpik Osleidys Menendez alirusha mkuki kwa masafa ya mita 71.70.

Msichana wa Ujerumani Christina Obergfoll aliondokea na medali ya fedha .

BUNDESLIGA:

Bundesliga-ligi ya Ujerumani ilikamilisha kalenda yake ya mwishoni mwa wiki kwa chipukizi FC cologne jana kuichezesha Stuttgart kindumbwe-ndumbwe na kuizaba mabao 3-2.Cologne ikicheza na wachezaji 10 tu dakika 19 za mwisho, kabla ikiongoza kwa mabao 3:0.

Mzambia Andrew Sinkala alitolewa nje ya uwanja na rifu baada binafsi kuchezewa ngware.Stuttgat ilikosa kutia bao la penalty.Kocha wao mtaliana Giovanni Trapattoni amevunjwa moyo na pigo hilo asilolitazamia.Kocha wa FC Cologne Uwe Rapolder kwa upande wake,amesema wamefurahi kuondoka Stuttgart na pointi 3 .Kwa mara nyengine nahodha wao Lukas podolski alinawiri.

Katika mpambano wapili jana wa Bundesliga-Bremen iliilaza Mainz mabao 2:0.Klasnic aliufumania mlango wa mainz tayari mnamo dakika ya 21 kabla Miroslav Klose kufunga hesabu kwa bao la pili mnamo dakika ya 62 ya mchezo.

Jumamosi tayari mabingwa watetezi Bayern Munich waliwaibisha wenyeji wao Bayer Leverkusen kwa mabao 5-2 nyumbani mwao.Schalke nayo ikatamba kwa mabao 2:1 mbele ya B.Dortmund.Borussia Möenchengladbach ilitoka suluhu bao 1:1 Wolfsburg.Berlin iliadhibu Frankfurt kwa mabao 2:0 huku Kaiserslauten ikinguruma kwa mabao 5-3 ya duisburg.Nüremberg ilitoka suluhu na Hannover 1:1.hamburg ilionea Bielefeld kwa kuichapa 2:0.

Munich inaongora orodha ya Ligi kwa pointi 6 kama Bremen,Hamburg,schalke na Fc Cologne, isipokua ina magoli zaidi kuliko timu nyengine zinazoifuata nyuma.

Mghana Michael Essien mwishoe, anajiunga na Chelsea ya Uingereza baada ya klabu yake bingwa ya Ufaransa Olympique Lyon kuregeza jana kamba na kumuachia kwenda Uingereza.Chelsea na Lyon zinakariobua kuafikiana kwa muujibu wa duru karibu na Lyon.Lyon awali ikidai kitita cha dala milioni 56 kumkomboa mghana huyo mwenye umri wa miaka 22.

Kesho asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu atie gongo mkutano uwanjani Amani Stadium,Zanzibar. Rais Amani Karume atafungua kesho rasmi dimba Kati ya Zanzibar na Kenya kuania kombe la chipukizi la CECAFA:

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW