MASHINDANO YA UBINGWA WA RIADHA HELSINKI
8 Agosti 2005MASHINDANO YA UBINGWA WA RIADHA DUNIANI MJINI HELSINKI:
Leo bingwa wa Olimpik wa masafa ya mita 10.000 Kennenisa Bekele wa Ethiopia anaingia uwanjani jioni hii mjini Helsinki kutetea taji lake la masafa hayo na kupatia Ethiopia medali nyengine ya dhahabu baada ya ile ya nyumamosi pale wasichana 3 wa Ethiopia walipofuatana na kuzoa medali zote tatu-dhahabu-fedha na shaba:
Wakati Kennenisa Bekele wa Ethiopia atazamiwa kutamba jioni hii katika mita 10.000,finali 5 zinagawa medali za dhahabu hii leo:Mbali na mita 10.000 wanaume, mita 3000 kuruka viunzi wanawake ni miongoni mwa medali za dhahabu zitakazoaniwa.Baadae, Bekele atageukia mita 5000 kutimiza shabaha yake alioshindwa kuitimiza katika michezo ya mwaka jana ya olimpik mjini Athens-yaani kutwaa mataji yote 2:mita 5000 na 10.000.Halkadhalika, baada ya Muamerika Justin Catlin kutamba jana katika mita 100 wanaume, leo ni zamu ya wanawake:Mfaransa Christine Arron anatazamiwa mara hii kuwika baada ya kuweka rekodi mpya ya Ulaya masafa ya mita 100 ya sek.10.73 wakati wa michezo ya Budapest,1998.
Finali nyengine ni za kurusha nyumndo wanawake na kuruka juu high jump.
Katika kombe la klabu bingwa barani Afrika, klabu 2 za Misri-Al Ahli na Zamalek zimetia fora na zinakaribia kukata tiketi zao kwa nusu-finali ya kombe hilo.Mabingwa Enyimba kutoka Nigeria,ambao walipepesuka, sasa wamerudi kutia fora katika kiu chao cha kutwaa Kombe hilo la Afrika kwa mara ya tatu mfululizo.Al Ahli sasa inahitaji pointi 1 tu kuingia nusu finali baada ya kuongeza uongozi wao katika kundi A kwa pointi 6 kufuatia sare jana na Ajax Cape Town.
Zamalek iliparamia kileleni mwa kundi B ilipotoka nyuma na kuizaba Esperence ya Tunisia mabao 2:1.Zamalek inaongoza kundi lake kwa magoli ilioichapa Etoile du sahel-timu nyengine ya Tunisia.
Ama mabingwa Enyimba ya Nigeria ilitamba kweli jana ilipoizaba Raja Casablanca ya morocco 2:0.
Stadi wa dimba wa Ghana,Michael Essien atabidi kusalia kuichezea Olympique Lyon –klabu bingwa ya Ufaransa.Binafsi angependa kuihama na kujiunga na Chelsea-mabingwa wa Uingereza.Chelsea ilipewa muda hadi mwishoni mwa wiki kuamua kumkomboa Essien kwa kima cha Euro milioni 45-sawa na dala milioni 56.Chelsea haikujitolea kulipa kitita hicho.
BUNDESLIGA-Ligi ya Ujerumani ilianza mwishoni mwa wiki kwa mshindo mkubwa:mabingwa watetezi Bayern Munich walifungua dimba katika uwanja wao mpya wa Allianz Arena kwa kuikumta Borussia Mönchengladbach mabao 3:0.Siku ya pili yake hapo jumamosi, mabingwa wa zamani Werder Bremen waliparamia kileleni mwa Bundesliga walipoizamisha jahazi ya Armenia Bielefeld kwa mabao 5-2.Muafrika Kusini Zuma akicheza kwa mara ya kwanza katika Bundesliga, aliipa Bielefeld bao lake la kwanza katika Bundesliga.
Bayer Leverkusen ikijiweka nafasi ya pili ya orodha ya Ligi ilipoizaba Frankfurt mabao 4-1.FC Cologne ikicheza na jogoo lao Lukas podolski iliondoka na ushindi wa bao 1:0 nyumbani dhidi ya Mainz.Schlake nayo ikawika mbele ya Kaiserslauten 2:1.