1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mashirika ya ndege yasimamisha safari za Mashariki ya Kati

3 Oktoba 2024

Mashirika kadhaa ya ndege yamesimamisha safari zake Kwenda na kutoka Iraq, Iran na Jordan kutokana na kuongezeka kwa machafuko katiuka eneo la ukanda wa mashariki ya kati.

Qantas Australia Pacific Blue
Picha: BARBARA WALTON/dpa/picture alliance

Mashirika kadhaa ya ndege yamesimamisha safari zake Kwenda na kutoka Iraq, Iran na Jordan kutokana na kuongezeka kwa machafuko katiuka eneo la ukanda wa mashariki ya kati.  
Hatua hiyo ni baada ya mashambulio ya makombora ya Iran dhidi ya Israel na ambayo imesababisha hofu ya uwezekano wa kuzuka vita vikubwa. Shirika la ndege la Emirates limesimaisha safari zake kwa muda wa siku tatu kwenda kwenye miji ya Basra, Baghdad, Tehran.

Soma pia: Miito yaendelea kutolewa ili kutoutanua mzozo wa Mashariki ya Kati

Na Vilevile Shirika la ndege la Qatar limesitisha kwa muda safari zake za ndege kwenda na kutoka Iraq, Iran na Lebanon.
Mnamo siku ya Jumanne, shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa, lilisema limesitisha safari za ndege kwenda Beirut na Tehran hadi Novemba 30 na safari zake kuelekea Tel Aviv zitasitishwa hadi Oktoba 31.