Israel yakataa kuruhusu upelekaji misaada Gaza
12 Novemba 2024Matangazo
Taarifa ya mashirika hayo inasema hali inazidi kuwa mbaya zaidi huko Gaza kuliko wakati wowote katika mzozo huo uliodumu kwa miezi 13.
Mwezi uliopita, utawala wa Rais Joe Biden ulitoa wito kwa Israel kuruhusu upelekaji wa chakula na misaada mingine ya dharura katika Ukanda wa Gaza, na kutoa muda wa siku 30 ambao umemalizika siku ya Jumanne.
Mashambulizi ya Israel yauwa zaidi ya watu 20 Lebanon
Marekani ilionya kuwa kushindwa kutimiza matakwa hayo, kunaweza kusababisha sheria za Marekani zinazoitaka kupunguza uungwaji mkono wa kijeshi.
Israel ilitangaza hatua kadhaa kuboresha hali hiyo lakini maafisa wa Marekani hivi karibuni waliashiria kwamba Israel bado haijafanya vya kutosha katika kushughulikia suala hilo.