1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Asilimia 60% ya vijana nchini humo hawana ajira.

Ibrahim Swaibu
1 Mei 2020

Mashirika hayo yana wasiwasi kuhusu hatma ya watu maskini na wakimbizi ambao wameathirika zaidi kutokana na mikakati ya serikali katika kukabiliana na COVID-19

Irak Coronavirus
Picha: picture-alliance/AP Photo/A. Khalil

Kufikia Aprili 30  serikali ya Lebanon imeweza kudhibiti usambaaji wa virusi vya Corona, kufuatia kuwekwa kwa mikakati ya kuzuia virusi hivyo, hiyo ni kwa mujiibu wa vyombo vya habari ambavyo pia vimeripoti kuwa hatua hizo kali za serikali katika kupambana dhidi ya COVID-19 imesababisha kudorora kwa hali ya maisha ya watu maskini na wakimbizi nchini humo.

Mnamo Aprili 27 idadi ya watu 707 ndio waliothibitishwa kuwa na mambukizi wa virusi vya Corona huku wengine 24 wakifariki kutokana na COVID-19. Kwa mujiibu wa watafiti katika chuo kikuu cha Johns Hopkins. Wataalamu wanasema nchi hiyo ya Mashariki ya Kati bado inaweza kuzuia hali mbaya ya janga la virusi vya Corona linaoukabili ulimwengu mzima.

Idadi ya mambukizi ya virusi vya Corona kuwa ndogo ni kutokana na serikali kuchukua hatua dhabiti zikiwemo kufunga maeneo ya umma kama shule, vyuo vikuu na migahawa. Wataalamu hao wameongeza. Awali mnamo Machi 9, Lebanon ilichukua hatua ya kusitisha vikao vya bunge.

Wafanyakazi wa shirika la kutoa misaada wakipakia chakula na vifaa vya usafi kwenye gari kuzipelekea familia maskini katika mji wa Tripoli kaskazini mwa LebanonPicha: CARE/Paul Assaker


Hata hivyo mashirika ya kutoa misaada nchini humo yameeleza wasiwasi wake kuhusu hatma ya watu maskini pamoja na wakimbizi ambao wameathirika zaidi kutokana na mikakati mikali ya serikali katika kukabiliana na janga hilo.

''Kutokana na hali kwamba watu hawafanyi kazi tena, wengi wao wanazidi kukabiliwa na umaskini, amesema Bujar Hoxha, mkrugenzii mkuu wa shirika la kutoa msaada nchini Lebanon la CARE International. Bujar ameambia DW kuwa janga la COVID-19 limezidi kusambaratisha hali nchini Lebanon ambayo tangu mwaka jana uchumi wake umekuwa chini huku idadi kubwa ya raia wakikosa ajira.

''Kwa sasa mimi na watoto wangu tunapata chakula, lakini sina uhakika iwapo  kesho au baada ya siku mbili ama katika kipindi cha wiki moja au mbili tutapata chakula. Na si mimi pekee, hali ni hivyo kwa kila mtu. Sasa nina wasi kubwa kuwa familia yangu itakumbuwa na njaa hata kuliko Corona. amesema Hassan Zeitadereva kutoka Lebanon


Kulingana na takwimu rasmi za serikali mnamo mwaka huu  2020, asilimia 45% ya Walebanon wataishi kwa umaskini na wengine asilimia 22% kuishi kwa umaskini uliokithiri. Lebanon inapambana na janga la COVID-19 wakati deni lake likikua kwa asilimia 170% ya pato jumla la kitaifa huku  ikikabiliwa na uhaba wa sarafu, hali ambayo inaweza kusababisha kuanguka kwa baadhi ya benki zake.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari kiwango cha ukosefu wa ajira kimepanda kwa asilimia 30% na zaidi ya asilimia 60% ya vijana nchini humo wakiwa hawana ajira.

Wakati huo huo, kambi yenye wakimbizi wengi ya Wavel imewekwa chini ya karantini baada ya mtu mmoja kuthibitishwa kuwa na mambukizi ya virusi vya Corona mnamo Aprili 22. Hata hivyo kufikia sasa watu wanne pia wamegundulika kuwa na ugonjwa wa COVID-19 na kuongeza hofu katika kambi hiyo yenye idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Palestina.

Mashirika ya kutoa misaada yana wasiwasi kwamba huenda virusi hivyo vikasambaa pia katika kambi za mamilioni ya wakimbizi kutoka nchini Syria ijapokuwa kufikia sasa, bado hakujatokea kisa chohote cha virusi hivyo hatari kwenye kambi za wakimbizi  kutoka nchini Syria.

Chanzo : DW