1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashirika ya misaada yahofia athari za vurugu Kongo

9 Februari 2024

Mashirika ya misaada yameelezea wasiwasi kuhusu athari za vurugu zinazoongezeka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako mapigano mapya yalizuka siku ya Alhamisi (Februari 8).

Wakimbizi wa ndani Kongo
Kambi ya wakimbizi wa ndani ya Rusayo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Picha: Alexis Huguet/AFP

Mapigano kati ya waasi wa kundi la M23 na vikosi vinavyoiunga mkono serikali ya Kongo, ambayo yameendelea kwa zaidi ya miaka miwili, yamezidi hasa katika mkoa wa Kivu Kaskazini, ambako raia wanakabiliwa na mashambulio ya mabomu, maelfu wakilaazimika kukimbia na watoto kupotea.

Soma zaidi: Jeshi la DR Kongo lawazuiwa waasi wa M23 kuutwaa mji wa Sake

Jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa nchini Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo limesema katika taarifa kwamba ongezeko la waathirika wa kiraia na matumizi ya silaha nzito katika maeneo ya raia, ikiwemo kambi za wakimbizi linatia wasiwasi.

Soma zaidi: Wanne wauawa, 25 wajeruhiwa kwa mabomu ya M23

Mapigano hayo yamesababisha uhamaji mkubwa kuelekea maeneo kadhaa, na kuchochea hatari ya wale waliolazimika kukimbia na jamii za wenyeji wao.

Soma zaidi: Jeshi la DRC lapambana na M23 Kivu Kaskazini

Jukwaa hilo ambalo linawakilishi zaidi ya mashirika 120 ya kimataifa yanayoendesha shughuli zake Kongo, limetaka hatua za haraka kuwalinda raia na kuhakikisha uwepo wa njia za kiutu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW