1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashirika yataka Diallo aachiwe huru

4 Desemba 2023

Mashirika yasio ya kiserikali ya Afrika Magharibi yametoa wito kuachiliwa mara moja kwa mwanaharakati wa kutetea haki za binaadamu wa Burkina Faso, Daouda Diallo, aliyetekwa nyara mjini Ouagadougou.

Daouda Diallo
Mtetezi wa haki za binaadamu aliyetekwa nchini Burkina Faso, Daouda Diallo.Picha: Sophie Garcia/AP/picture alliance

Muungano wa mashirika hayo umesema Diallo alitekwa nyara siku ya Ijumaa (Disemba 1) na watu waliovalia nguo za kiraia nje ya ofisi za serikali mjini Ouagadougou.

Mashirika hayo yameeleza kuwa hakujatolewa taarifa zozote za Diallo au maelezo juu ya sababu za kutekwa kwake na yametoa wito wa kuachiliwa pamoja na kuhakikisha usalama wake.

Soma zaidi: Mali, Niger na Burkina Faso zakusudua kuunda shirikisho

Kwa mujibu wa shirika la Human Rights Watch, Diallo ambaye ni mshindi wa tuzo ya Martin Ennals mnamo mwaka 2022 inayotolewa kwa watetezi wa haki za binaadamu, alikuwa mmoja kati ya wakosoaji wakuu wa serikali ya Burkina Faso ambaye hivi karibuni, alitakiwa kujiunga na jeshi la nchi hiyo katika vita dhidi ya wapiganaji wa itikadi kali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW