kwa 'ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu'
13 Desemba 2024Mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu yamedai kuwepo kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu karibu na mradi mkubwa wa mafuta unaoendelezwa nchini Uganda na Tanzania na kampuni ya mafuta ya Ufaransa, TotalEnergies pamoja na ile ya China ya CNOOC.
Ripoti ya kurasa 100 iliyotolewa jana na Shirikisho la Kimataifa la Haki za Kibinadamu (FIDH), Mwitikio wa Kiraia juu ya Mazingira na Maendeleo (CRED) na Mawakili Wasio na Mipaka, imesema kumekuwa na hatua za usalama zisizo na usawa, ukandamizaji, ukiukwaji wa haki za kumiliki ardhi, kufurushwa kwa nguvu pamoja na rushwa wakati wa mradi huo.
Ripoti hiyo imedai kuwa wanajeshi wa Uganda wamezinyanyasa jamii za wavuvi.
Pia imerekodi unyanyasaji wa kingono na kijinsia uliofanywa na wanajeshi hao na wafanyakazi wa kampuni hiyo ya mafuta.
Serikali ya Uganda imeishtumu ripoti hiyo na kuitaja kuwa madai yasiokuwa na msingi.
Kampuni ya TotalEnergies pia imeipinga ripoti hiyo.