1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEthiopia

Mashuhuda wasema mapigano ya kikabila Ethiopia yaua raia

26 Januari 2023

Mashuhuda kadhaa wameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba raia wengi pamoja na wapiganaji wamekuwa wakiuawa.

Äthiopien Soldaten der äthiopischen Nationalen Verteidigungskräfte (ENDF)
Picha: AMANUEL SILESHI/AFP/Getty Images

Makabiliano hayo yaliibuka siku ya Jumamosi katika mji wa Jewuha lililopo jimbo la Amhara. Mmoja ya mashuhuda ambaye hakutaka kutambulishwa aliliambia shirika hilo la habari kwamba wanamgambo wanaodhaniwa kutoka Jeshi la Mapinduzi la Oromo, waliishambulia kambi iliyotumiwa na vikosi maalumu vya Amhara na kuwaua zaidi ya wanajeshi wake 20.

Shuhuda mwingine katika mji wa Ataye, katika jimbo la Amhara amedai kwamba mapigano kati ya OLA na vikosi hivyo maalumu vya Amhara yalikuwa yakiendelea na maelfu ya raia wamekimbia.

Serikali ya jimbo la Amhara imethibitisha jana kuhusu mapigano hayo na kusema wanajeshi wa jeshi la shirikisho, polisi na vikosi maalumu vya Amhara wanapambana kurejesha utulivu, huku wasemaji wa polisi ya shirikisho na serikali wakikataa kuzungumza. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW