Katika jimbo la uchaguzi la Duisburg Hochfeld magharibi mwa Ujerumani, ni mtu mmoja tu kati ya watano hujitokeza kupiga kura. Katika kitongoji hicho maskini, ni wachache walio na nia ya kushiriki katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Ujerumani mwishoni mwa mwezi Septemba, kwa sababu wamepoteza imani katika siasa. #Kurunzi