1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano ya Msumbiji yaathiri masoko ya ndani na nje

14 Desemba 2024

Masoko ya Maputo ambayo kwa kawaida yanakuwa na shughuli nyingi yameendelea kuwa tupu kuliko kawaida huku maduka ya vyakula vikuu kama vile viazi na vitunguu yakiwa hayana chochote na wafanyabiashara wana wasiwasi

Mosambik Maputo 2024 | Proteste legen Autoverkehr lahm
Picha inaonyesha siku ya mwisho kinyang'anyiro cha uchaguzi mjini Maputo.Picha: Romeu da Silva/DW

Halli hiyo inadhihirika ikiwa ni takribani miezi miwili ya machafuko ya baada ya uchaguzi am,bay mara kwa mara huzuia uagizaji bidhaa kutoka Afrika Kusini. Maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Msumbiji ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 100, kulingana na mashirika ya kiraia yamesababisha ugumu wa kuingia katika maeneo ya katikati ya jiji. Kadhalika yametatizoa safari katika mpaka mkuu na Afrika Kusini, njia muhimu ya uagizaji bidhaa ambapo katika majuma yaliopita ufungwa mara kwa mara hali inayo tatizo mwenendo wa hali ya uchumi kwa nchi zote mbili. Viazi, karoti, vitunguu na mazao mengine yanayoletwa kutoka Afrika Kusini ni vigumu kupatikana sokoni. Kiongozi mkuu wa upinzani Venancio Mondlane Jumatatu anatazamiwa kutangaza wimbi jipya la maandamano.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW