1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Allegri aihama Juventus

20 Mei 2019

Juventus Jumapili walikabidhiwa rasmi kombe lao la ubingwa wa ligi ya nchini humo Serie A baada ya kutoka sare ya bao moja na Atalanta.

Fußball |  Juventus Turin vs AC Florenz | Ronaldo
Picha: imago//ImagePhoto/M. Gribaudi

Lakini wanampoteza kocha wao Massimiliano Allegri ambaye anaondoka baada ya kuhudumu kama mkufunzi kwa kipindi cha miaka mitano.

Allegri mwenye umri wa miaka hamsini na moja anasema lakini kuwa anaondoka ila hana kinyongo na yeyote.

"Tumezungumza na wakuu wa klabu na tukaelezana kile kilicho bora kwa Juventus na mustakabali wake. Baada ya hapo wakuu wakaitathmini hali nzima na ikaamuliwa ni vyema kwamba nisiwe kocha wa klabu hii msimu ujao. Hili halibadilishi chochote kwasababu hali ya maelewani na Rais Agnelli, wakurugenzi Pavel Nedved na Fabio paratici bado yanasalia kuwa mazuri kabisa," alisema Allgeri.