1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maswali na majibu bungeni mara ya kwanza Ujerumani

Sekione Kitojo
7 Juni 2018

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani  wameandika kikao cha maswali na majibu bungeni ambapo kansela Merkel aliyajibu maswali ya wabunge, uchaguzi nchini Uturuki, pamoja na Mjerumani aliyekwenda katika kituo cha ISS angani.

Deutschland, Berlin:  Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) beantwortet erstmals im Rahmen einer Fragestunde die Fragen der Abgeordneten
Kansela wa Ujerumani akihutubia bunge katika kipindi cha maswali na majibuPicha: picture-alliance/dpa/B. von Jutrczenka

Mara  nyingine wabunge  walinapaswa  kufanya  utafiti  kwanza  kabla  ya kuuliza  maswali. Hata  hivyo  inaonekana  kwamba  wabunge  kama inavyofahamika  walikuwa  wanajipasha  moto tu. Hakukuwa  na mjadala  mkali  katika  kikao  hiki  cha  maswali  na  majibu. Ndio sababu  kansela  aliweza  hata  kuwaaga  wabunge  kwa  kuwafinyia jicho  na  kusema , "nitakuja  tena". Huenda  hiyo  ni  ishara  ya kuwatuliza.

Gazeti  la Rhein-Zeitung  la  mjini  Koblenz  likiandika  kuhusiana  na tukio  hilo  la  maswali  na  majibu  bungeni , linasema wabunge wamepoteza  fursa, kumhoji  kwa  kina  kansela. Mhariri  anaandika:

Ili kikao  hicho  cha  maswali  na  majibu  kivutie  zaidi,  na  kuweza kufahamisha  zaidi , wauliza  maswali  walipaswa kuwa  na  ufahamu mkubwa  zaidi  na  kuuliza  maswali  magumu. Ilipaswa  iwe  ni mjadala, mazungumzo  yenye  mapambano,  na  mivutano. Makundi ya  wabunge  yalipaswa  kuwa  werevu  zaidi, na  kulenga  katika mada  moja  zaidi  na  kuuliza  maswali  zaidi  ya  kuchokonoa na magumu. Maswali  aliyotupiwa  kansela  pamoja  na  mawaziri yalikuwa  kama  kumsalimia  tu. Mfumo  huo  kwa  kweli  haujakuwa wa  mafanikio.  Wabunge  wanahitaji  uhuru  zaidi, ili  kuweza  kuuliza maswali mazito  na  kupambana na  majibu ya  juu  juu  ya yanayotolewa  na  kansela.

Mambo  mawili  muhimu  hayapaswi  kupuuziwa:  anaandika  mhariri wa  gazeti  la  Mannheimer  Morgen  , kuhusiana  na  uchaguzi  wa rais  na  bunge  nchini  Uturuki. Mhariri  anaadika:

Kwanza ni  kwamba  rais  Erdogan  na  chama  chake  cha  AKP amefanikiwa  hapo  nyuma  kupitia  mageuzi  kuibadilisha Uturuki kiuchumi  na  kuleta  hali  bora  kwa  wananchi wake. La  pili  ni kwamba  mbali  na  kuleta  hali  ya  kuwa  ni  kiongozi  anayeelekea kuwa mtawala  anayejilimbikizia  madaraka lakini  ni  mmoja  kati  ya wale  walioleta uthabiti  nchini  mwake. Upinzani  umegawanyika, Waturuki  katika  miongo  iliyopita  walishuhudia  mapinduzi  kadhaa na  kuvunjika  kwa  serikali. kutokana  na  hayo  kunatokea  hali  ya wasi wasi  katika  mataifa  jirani  kama  vile  Syria ama  hata  Iraq.

Mada  ya  mwisho  inahusu  Mjerumani Alexander Gerst  aliyesafiri kwenda  katika kituo  cha  anga  cha  kimataifa angani ISS. Gazeti  la Mittelbayerische Zeitung  la  mjini  Regensburg linaandika:

Gerst  ni mtu  anayeleta  furaha  kwa  shirika  la  Ulaya  la  mambo ya  anga ESA pamoja  na  shughuli  za  safari  za  anga  za  juu  kwa jumla. Kuna  watu  kama  yeye  ama  mwanaanga  wa  canada anayependelea  kupiga  gitaa  Chris Hadfield , ambao  wamefanikiwa , kuamsha  hamasa  kubwa kwa  watu  wengi , kuhusu  mambo  ya anga  za  juu  na  utafiti   katika  kituo  cha  ISS. Ndio  sababu  ni muhimu , kwa  kuwa  mpango  wa  safari  za  anga  za  juu  ni  ghali , na  baadhi  hujiuliza  iwapo  fedha  hizo  zisingetumika  vizuri  hapa ardhini.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / inlandspresse /

Mhariri: Iddi Ssessanga