UchumiAfrika
Mataifa manne ya Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/25
14 Juni 2024Matangazo
Nchini Kenya Waziri wa Fedha Njuguna Ndung'u aliwasilisha makadirio ya bajeti ya kiasi shilingi Trilioni 4 inayojumuisha mapendekezo ya nyongeza ya kodi na ushuru ambayo wakosoaji wanasema yatazidisha mzigo kwa raia wa kawaida.
Serikali ya Tanzania yenyewe imependekeza makadirio ya shilingi trilioni 44.39 kwa ujao wa fedha huku Bunge la Uganda tayari limeidhinisha bajeti ya shilingi trilioni 72.13 iliyosomwa jana. Rwanda nayo iliweka mezani bajeti ya kiasi faranga Trilioni 5.69 ikiwa ni nyongeza ya asilimia 11.2 ikilinganishwa na ya mwaka uliopita.
Benki ya Maendeleo ya Afrika inakadiria uchumi wa kanda ya Afrika Mashariki utakua hadi kufikia asilimia 5.7 mwaka ujao hali inayoleta matumaini baada ya kipindi cha ukuaji duni wa uchumi.