1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa ya Baltic NATO yajadili usalama mkutano wa Helsinki

14 Januari 2025

Nchi za eneo la Baltic na ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Kujihami - NATO zinajadili usalama katika kanda hiyo kwenye mkutano wa kilele hii leo mjini Helsinki, Finland.

Mkutano wa mataifa ya Baltic
Mkutano wa mataifa ya BalticPicha: Henrik Montgomery/TT/REUTERS

Katika matukio ya karibuni, nyaya kadhaa za umeme na za intaneti zinazopita chini ya Bahari ya Baltic zilidaiwa kukatwa makusudi.

Madhumuni kuu ya mkutano huo ni kutafuta njia za kulinda vyema miundombinu muhimu katika Bahari ya Baltic na kukabiliana na tishio la kile kinachoitwa meli za kivuli za Kirusi ambazo husafiri kisirisiri.

Soma pia: NATO, Urusi wafanya luteka mkabala bahari ya Baltiki

Hii inahusu meli ambazo Urusi hutumia kusafirisha mafuta, kwa mfano, ili kukwepa vikwazo vilivyowekwa kutokana na uvamizi wake wa Ukraine.

Mkutano huo unaongozwa na Rais wa Finland Alexander Stubb na Waziri Mkuu wa Estonia Kristen Michal. Viongozi wa nchi za NATO katika eneo la Baltic pia wanatarajiwa kuhudhuria, zikiwemo Denmark, Ujerumani, Latvia, Lithuania, Poland na Sweden. Mkuu wa NATO, Mark Rutte, pia atahudhuria.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW