1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa ya G7 yalaani kuvurugwa kwa demokrasia ya Hong Kong

21 Desemba 2021

Kundi la mataifa yenye kuvungu ya kiviwanda dunia G7 yamelaani hatua ya China katika kuvuruga demokrasia ya Hong Kong.

Hongkong | Parlamentswahl Auszählung
Picha: Vernon Yuen/NurPhoto/picture alliance

Mataifa yenye nguvu duniani yamelaani mfumo wa uchaguzi wa bunge la Hong Kong uliochujwa vikali kwa kusema sheria zilizowekwa na China zilipunguza uwezekano wa kuwachagua wabunge moja kwa moja na kudhibti nani hasa ambaye anapaswa kuchaguliwa.

Kumekuwa na maandamano makubwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita katika eneo la Hong Kong, kadhia ambayo imetokana na kile kinachotajwa kuwa ni ubinywaji wa kidemokrasia unaoratibiwa na China Bara.

Athari za sheria ya usalama wa taifa ya China.

Wapiga kura wakiwa katika foleni Hong KongPicha: Vincent Yu/AP/picture alliance

Taifa hilo limeweka sheria ya usalama wa taifa katika eneo hilo lilikuwa koloni la Uingereza ambayo zimefanya upinzani kuwa uhalifu pamoja na kuweka kanuni ambazo zinachunguza itikadi ya yeyote katika ofisi ya umma.

Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la mataifa saba yaliostawi zaidi kiviwanda G7 wameonyesha wasiwasi wao juu ya mmomonyoko wa demokrasia katika mfumo wa uchaguzi.

Mawaziri wa mambo wa nje wa Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza na Marekani wameihimiza China kurejesha imani kwa taasisi za kisiasa na kukomesha ukandamizaji kwa wanaharakati wanaopigania demokrasia.

Umoja wa Ulaya wasema uchaguzi wa Hong Kong kielelezo cha uharibifu.

Mawaziri wa mambo ya nje wa matiafa ya G7Picha: Olivier Douliery/AP Photo/picture alliance

Naye mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borell amesema katika taarifa kuwa uchaguzi huo ni hatua nyengine ya kuvunjwa kwa sera ya nchi moja mifumo mwili na kutoa wito wa kuheshimiwa kwa haki za binadamu Hong Kong.

Katika taarifa yao ya awali, Uingereza, Marekani, Canada, Australia na New Zealand zilitoka kalipio kali kuhusu mfumo huo mpya zikisema mabadiliko hayo yaliondoa upinzani wowote wa maana wa kisiasa katika eneo la Hong Kong.

Uchaguzi wa kwanza chini ya utaratibu mpya wa ulifanyika Jumapili, hatua ambayo kihistoria ilionekana kutekelezwa kwa idadi ndogo ya watu.Na idadi ya waliopaswa kuchaguliwa walipunguzwa kwa nusu ya watu 22. Idadi ambayo inaelezwa kuwa ndogo zaidi tangu tafa hilo likabidhiwe kwa China kutoka katika himaya ya Uingereza mwaka 1997.

Uchaguzi wa bunge wa 2016 asilimia 58 ya wapiga kura ilijitokeza, wakati ambapo 2019, uchaguzi ambao wapigania demokrasia walishinda kwa kishindo walijotokeza asilimia 71 ya watu.

Chanzo: AFP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW