1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa ya Bahari ya Kaskazini kukuza nishati ya upepo

26 Januari 2026

Mataifa tisa ya Ulaya yamekubaliana leo kukuza uzalishaji wa nishati ya upepo katika Bahari ya Kaskazini, kwa lengo la kuongeza nishati safi kwa mazingira na kupunguza utegemezi wa Urusi na mataifa mengine ya kigeni.

 Berlin 2025 | Waziri wa uchumi na nishati wa Ujerumani Katherina Reiche
Waziri wa uchumi na nishati wa Ujerumani Katherina Reiche Picha: Christoph Soeder/dpa/picture alliance

Mataifa tisa ya Ulaya yamekubaliana leo kukuza uzalishaji wa nishati ya upepo katika Bahari ya Kaskazini, kwa lengo la kuongeza nishati safi kwa mazingira na kupunguza utegemezi wa Urusi na mataifa mengine ya kigeni.

Makubaliano hayo yamefikiwa leo katika mkutano wa tatu wa nchi zinazopakana na Bahari ya Kaskazini unaofanyika Hamburg, Ujerumani. Waziri wa uchumi na nishati wa Ujerumani Katherina Reiche amesema kuwa.

"Lengo letu ni kuendeleza hifadhi kubwa zaidi ya nishati duniani, na manufaa ya upanuzi huu yako wazi: tunaongeza usalama wa upatikanaji wa nishati, tunaimarisha sekta yetu ya baharini, tunaongeza thamani ya kiuchumi, na ajira bora zenye viwango vya juu"

Ujerumani, Ufaransa, Uingereza na Denmark ni miongoni mwa nchi zilizotia saini makubaliano ya kuifanya Bahari ya Kaskazini kuwa hifadhi kubwa zaidi ya nishati safi duniani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW