1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJordan

Mataifa ya kiarabu yahofia uhamisho mpya wa Wapalestina

25 Oktoba 2023

Muonekana wa mahema katika miji ya Wapalestina ilioachwa bila makaazi Ukanda wa Gaza unaokabiliwa na vita umeibuwa kumbukumbu mbaya ya kihistoria kwa mataifa ya kiarabu yanayopakana na Israel ya Misri na Jordan.

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi akiwa na Mwanamfalme wa Jordan Hussein
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi akiwa na Mwanamfalme wa Jordan HusseinPicha: Yousef Allan/Jordanian Royal Palace/AFP

"Hivi ndivyo Nakba ilivyoanza," linasema kundi la utetezi wa haki lenye makao yake huko Gaza la Al Mezan, likiangazia wasiwasi wa kikanda kwamba Israel inapanga kulisafisha kabisa eneo hilo la pwani.

Nakba ama "janga" ndivyo namna ulimwengu wa Kiarabu unavyoelezea namna Wapalestina 760,000walivyolazimishwa kuondoka, wakati wa vita vilivyochochea kuanzishwa kwa taifa la Israel miaka 75 ijayo.

Mashaka ya historia kama hayo kujirudia yameendelea kuongezeka wakati Israel ikiendeleza vita vyake dhidi ya kundi la wanamgambo la Hamas, tangu walipowaua karibu watu 1,400 katika shambulizi ya Oktoba 7, kusini mwa Israel.

Na, tahadhari iliyotolewa na Israel ya kuwahamisha watu kaskazini mwa Gaza, huku kukiwa na minong'ono juu ya uvamizi wa ardhini imeibua wasiwasi mkubwa wa kihistoria, wakati watu milioni moja wa Gaza wakiwa tayari wamelazimika kuyakimbia makazi yao. 

Soma pia:Mataifa ya kiarabu yalaani shambulizi la Israel katika ukanda wa Gaza

Misri nayo imeruhusu malori ya misaada ya kiutu kuingia Gaza kupitia kivuko cha Rafah baada ya Israel kusitisha mashambulizi kuelekea upande wa Palestina chini ya makubaliano yaliyosimamiwa na Marekani.  

Lakini wakati huo huo inahofu kwamba hatua hiyo ya kufungua milango huenda ikawezesha mipango ya Israel ya kuwalazimisha Wapalestina wengi kuondoka.

Kituo cha Al Mezan kimesema picha kama hizo za mahema mipakani, zinaweza kumpa msisimko mtu yoyoteanayejua historia ya Wapalestina, na namna Nakba ilivyoanza.

Limesema, Wapalestina wengi wanaona bora kufia Gaza badala ya kuwa wakimbizi tena.

Misri yahofia usalama kuwapokea Wapalestina

Israel imesisitiza kwamba agizo la watu kuhama kaskazini mwa Gaza linalenga kuwaepusha raia dhidi ya mashambulizi wakati itakapokuwa ikiwakabili Hamas pamoja na kuwaokoa mateka zaidi ya 220. 

Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi akifungua mkutano wa amani kuhusu mzozo wa Israel na kundi la Hamas la PalestinaPicha: Khaled Desouki/AFP/Getty Images

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi amesisitiza kwamba Israel ina jukumu kwa ajili ya raia wa Palestina chini ya sheria ya kimataifa.

Amenukuliwa wakati fulani akisema kama wazo ni kuwaondosha kwa nguvu, kutakuwa na "Negev" akimaanisha ardhi kame katika eneo la kusini mwa Israel, na kwa upande mwingine anahofia usalama ikiwa itawahifadhi wakimbizi wa Palestina.

Kuwepo kwa wakimbizi wa Kipalestina na makundi ya wanamgambo hapo awali kuliziingiza nchi zilizowahifadhi katika migogoro, Jordan katika miaka ya 1970 na Lebanon katika miaka ya 1980.

Soma pia:Ajenda ya mahusiano kati ya Israel na mataifa ya kiarabu

Huko Jordan, ambako kuna Wapalestina wengi, hayati, Mfalme Hussein katika miaka ya 1970 aliwashutumu wapiganaji wa fedayeen wa Palestina kwa kujenga "nchi ndani ya nchi" na kutaka kuchukua taifa lao.

Ili kuzuia hili, mashambulizi ya Black September huko Jordan yalikisukuma Chama cha Ukombozi wa Wapalestina, PLO chini ya Yasser Arafat kuondoka Jordan na kwenda Lebanon.

Na hapo ndipo vyama vya kikristu vya Lebanon vilipoanza kupambana na PLO.

Arafat na wapiganaji wakewalilazimika kuondoka tena baada ya Israel kuivamia kikamilifu Lebanon, 1982.

Uongozi wa PLO ulitawanyika hadi Tunisia na Yemen, huku maeneo yaliyokaliwa ya Wapalestina yakigubikwa na uasi wa kwanza kabisa ama intifada, mwaka 1987.

Jitihada za kimataifa kumaliza mzozo 

Makubaliano ya Oslo ya 1993 yalikusudia kupatikana kwa taifa la Palestina, lakini ndoto hiyo ilififishwa na mazungumzo mazito yaliyokwama kwa muongo mmoja uliopita.

Idadi ya wakimbizi wa ndani Gaza yaongezeka kwa kasi

02:41

This browser does not support the video element.

Wazo la kuwa na nchi mbadala ya Wapalestina liliibuka tena chini ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, ambaye mpango wake wa amani, uliokataliwa na Wapalestina kwa madai uliegema upande wa Israel, ulipendekeza eneo la viwanda huko Sinai kuibua nafasi za kazi kwa watu wa Gaza. Wachambuzi wanasema hata Cairo ingeupuuza.

Soma pia:Iran yapinga mahusiano kati ya Israel na mataifa ya kiarabu

Rasi ya Sinai, iliyokaliwa na Israel tangu mwaka 1967, lilikuwa ni eneo la mapigano ambako wanajeshi wengi wa Misri walikufa, kabla ya Cairo kulirejesha chini ya makubaliano ya amani na Israel ya mwaka 1979.

Sisi anaonya kwamba, ikiwa huko siku za usoni makundi ya Wapalestina yaliyojihami kwa silahayaliyojikita kwenye ardhi yake wangetaka kuivamia Israel, basi historia ya amani "itayeyukia mikononi mwao."
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW