1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa ya kusini mwa Afrika yakabiliwa na janga la njaa

16 Oktoba 2024

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeonya kuwa mamilioni ya watu katika eneo la kusini mwa Afrika wanakabiliwa na njaa kwa sababu ya ukame wa kihistoria ambao unatishia kusababisha maafa makubwa ya kibinadamu.

Shirika la WFP lasema Mataifa ya kusini mwa Afrika yanakabiliwa na janga la njaa kutokana na ukame
Shirika la WFP lasema Mataifa ya kusini mwa Afrika yanakabiliwa na janga la njaa kutokana na ukamePicha: Sascha Steinach/dpa/picture-alliance

Miezi kadhaa iliyopita, nchi tano ambazo ni Lesotho, Malawi, Namibia, Zambia, na Zimbabwe, zilitangaza hali ya janga la kitaifa kutokana na ukame ambao umeharibu mazao na kuangamiza mifugo.

Katika taarifa iliyotolewa leo ikiwa ni Siku ya Chakula Duniani, WFP imesema kuwa Angola na Msumbiji pia zimeathirika pakubwa na kuonya kuwa mgogoro huo unatarajiwa kuongezeka kuanzia mwezi huu wa Oktoba hadi kipindi kijacho cha mavuno mnamo Machi au Aprili mwaka ujao.

Msemaji wa WFP katika eneo la kusini mwa Afrika Tomson Phiri, amesema ukame wa kihistoria, umeathiri zaidi ya watu milioni 27 kote katika eneo hilo la kusini mwa Afrika na kwamba takriban watoto milioni 21 wanakabiliwa na utapiamlo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW