Mataifa ya Magharibi; Urusi iwajibishwe kwa uvamizi Ukraine
3 Aprili 2024Katika tamko lililotolewa mwishoni mwa kongamano hilo la uhalifu wa kivita, mataifa hayo yalisema kuwa Urusi inapaswa kufunguliwa mashitaka kwa vita vyake vya uchokozi na kuwajibikia matendo yake.
Walioshiriki kongamano la uhalifu wa kivita
Kongamano hilo lilijumuisha mawaziri na waakilishi wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya pamoja na mahakama za kimataifa walioalikwa naUkrainena Uholanzi kujadili kuhusu uwezekano wa kufungua kesi ya uhalifu wa kivita unaodaiwa kufanyika nchini Ukraine.
Soma pia:Ukraine yakabiliwa na matatizo ya umeme kufuatia mashambulizi ya Urusi
Waakilishi wa mataifa yasiokuwa ya Ulaya kama vile Marekani , Canada na Australia pia walihudhuria.
Washiriki wa kongamano hilo, walisema kuwa wamejitolea kuhakikisha kuundwa kwa jopo maalumu la kuchunguza na kushitaki uhalifu uliofanywa na Urusi nchini Ukraine.