1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIran

Iran yawekewa vikwazo madai ya upelekaji makombora Urusi

11 Septemba 2024

Mataifa makubwa ya magahribi yametangaza orodha mpya ya vikwazo dhidi ya Iran wanayoituhumu kuipatia Urusi makombora ya masafa marefu ambayo inaaminika Moscow itayatumia dhidi ya Ukraine.

Moja ya makombora ya Iran
Moja ya makombora ya Iran.Picha: Morteza Nikoubazl/NurPhoto/picture alliance

Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimetangaza kuifuta mikataba yote ya sekta ya anga na jamhuri hiyo ya Kiislamu na kuliwekea vikwazo shirika la ndege la Iran Air. Mataifa hayo matatu yamesema hatua hizo zinachukuliwa kujibu uamuzi wa Iran wa kupuuza onyo la kutoipatia Urusi silaha.

Marekani kwa upande wake nayo imetangaza vikwazo vya pamoja na Uingereza dhidi ya watu inaowatuhumu kuratibu mipango ya kupeleka makombora ya Iran nchini Urusi.

Hata hivyo Iran yenyewe imesema madai yanayotolewa na nchi za magharibi ni "njama chafu" ya "kuwafumba macho na kuwapumbaza walimwengu" juu ya shehena ya silaha ambazo mataifa hayo zinaipatia Israel iliyo hasimu mkubwa wa Iran.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW