1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mataifa ya Magharibi yataka msaada wa kiutu kuingizwa Sudan

19 Oktoba 2024

Nchi za Magharibi zikiwemo Uingereza, Marekani, Ufaransa na Ujerumani, jana zilizitaka pande mbili zinazozozana nchini Sudankuruhusu kuingizwa nchini humo msaada unaohitajika haraka na mamilioni ya watu.

Uharibifu uliosababishwa na shambulizi la anga katika soko la  Al-Souk Al-Markazy mjini Khartoum, Sudan mnamo Oktoba 13, 2024, ambapo watu 23 waliuawa na zaidi ya 40 kujeruhiwa.
Uharibifu uliosababishwa na shambulizi la anga katika soko la Al-Souk Al-Markazy mjini Khartoum, SudanPicha: Volunteer Group South Khartoum Emergency Room/Xinhua/IMAGO

Nchi hizo zilitaka kuondolewa kwa vikwazo vya usafiri kwenye mpaka wa Adre kutoka Chad, ambako Umoja wa Mataifa unasema malori yake yanasubiri ruhusa ya kuingia Sudan.

Nchi hizo pia zilitoa wito wa kufunguliwa kwa njia zote za mpakani bila kuweko kwa vizuizi vyovyote, hatua ambayo awali ilikuwa imekubaliwa na pande hizo mbili zinazozozana.

Soma pia: Wakimbizi wa Sudan hatarini kutokana na mapigano: HRW

Katika tamko hilo, lililotiwa saini na Kamishna wa Ulaya wa Udhibiti wa Migogoro, nchi hizo zilisema  zinalaani kwamba licha ya dharura iliyoko, pande hizo za SAF na RSF zinaendelea kuzuia kuingizwa nchini humo kwa msaada wa kibinadamu.

Pande zote mbili zimeshtumiwa kwa uhalifu wa kivita ikiwa ni pamoja na kuwalenga raia na kuzuia msaada wa kibinadamu.