1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Msaada zaidi wa kuijenga upya Ukraine watolewa mjini London

21 Juni 2023

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema nchi yake imepanga kuipa Ukraine msaada wa ziada wa fedha wa euro milioni 416 ili kusaidia kuijenga upya nchi hiyo inayokabiliwa na vita.

London Ukraine Recovery Conference Baerbock
Picha: Thomas Koehler/photothek/picture alliance

Annalena Baerbock amesema kiwango hicho cha fedha kitasaidia kununua majenereta, chakula na mahema yatakayotumika kuwafadhi watu zaidi waliopoteza makaazi yao kufuatia vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraime. 

Tangu Urusi ilipoivamia jirani yake, tarehe 24 Februari, fedha zilizotolewa na Ujerumani kwa ajili ya kuisaidia nchi hiyo zimefikia dola bilioni 16.8. Baerbock amesema wanaisaidia Ukraine kuwekeza katika nishati mbadala na ufanisi wa nishati.

Katika mkutano huo mkutano huo wa nchi za Ulaya unaofanyika mjini London ulio na lengo la kuisadia Ukraine, waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken alitangaza pia kwamba, nchi yake itatoa euro bilioni 1.3 za ziada kuisaidia Ukraine, ambapo milioni 520 zinanuiwa kuelekezwa katika kukarabati mifumo ya usambazaji umeme ya taifa hilo ili kuifanya kuwa imara. Blinken amesema pamoja na masoko ya nishati, hatua iliyochukuliwa huenda ikaifanya Ukraine kuwa moja ya mataifa yanayotegemewa kuuza kiwango kikubwa cha nishati.

Mkutano wa kuijenga upya Ukraine kufungua pazia mjini London

Vijiji vitano vyakosa huduma muhimu ya umeme Ukraine

Catherine aliye na miaka 70 akiushikilia mshumaa, wakati moja ya kijiji chake kikikosa huduma ya umeme mjini KievPicha: Emilio Morenatti/AP/picture alliance

Wakati huo huo kumeshuhudiwa ukosefu mkubwa wa umeme katika maeneo mengi ya mji mkuu wa Ukraine Kiev, huku zaidi ya watu 100,000 wakiathiriwa na tatitzo hilo, hii ikiwa ni kulingana na utawala wa mji huo.

Kufeli kwa mfumo wa usambazaji umeme ndio sababu iliyotajwa ya mji huo pamoja na vijiji vingine vitano mjini humo kuwa gizani, na kukwamisha pia usafiri wa treni

Kulingana na serikali ya Ukraine, maeneo mengine ya mji yalikosa huduma hiyo muhimu ya umeme hapo jana baada ya ndege zisizokuwa na rubani kuishambulia Ukraine.

Hata hivyo maafisa walisema walifanikiwa kuzidungua ndege zote zilizorushwa kutoka Moscow.

Von der Leyen asema anaamini Ukraine itajiunga na EU

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, akiwa na rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Sergei Supinsky/AFP/Getty Images

Huku hayo yakijiri rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa ulaya Ursala von der Leyen amesema anaamini Ukraine siku moja itajiunga na Umoja huo. Umoja huo umesema tayari Ukraine imeshakamilisha mabadiliko mawili kati ya saba iliyowekewa kabla ya mazungumzo rasmi kuanza ya kujadili ombi la taifa hilo kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Urusi yaitahadharisha Ukraine kuhusu kuishambulia Crimea

Ukraine imefanya mabadiliko kwa kusitisha ushawishi wa kisiasa katika vyombo vya habari, na pia mabadiliko katika mahakama zake. Mwezi Oktoba  Uongozi wa Juu ya Ulaya unatarajiwa kutoa ripoti yake juu ya hatua zilizopigwa na Ukraine na kutoa maoni yake iwapo mazungumzo hayo yaanzishwe au la.

Ukraine yasema kijiji kimoja kimekombolewa upande wa kusini

Kwa hilo kutimia mataifa yote 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya wanapaswa kukubaliana. Poland na mataifa ya Baltic yanaiunga mkono Ukraine kujiunga na Umoja wa Ulaya huku Ujerumani na Uholazi ikitaka mchakazo mzima kutoharakishwa.

Chanzo: afp/ap/reuters/dpa

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW