Janga la ugonjwa wa kifaduro lafagia Ulaya
8 Mei 2024Matangazo
Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa barani Ulaya kimesema kuwa, wagonjwa 60,000 wa kifaduro wameripotiwa barani Ulaya ndani ya muda wa mwaka jana hadi robo ya kwanza ya mwaka huu huku watu 19 wakifariki dunia, wakiwemo watoto wachanga 11 na watu wazima wanane.
Soma pia: Watoto milioni 20 hawapati chanjo ya magonjwa hatari
Nchini Uingereza, kwa mfano, wataalamu wa afya wametahadharisha kuwa visa vya ugonjwa huo unaothiri zaidi mapafu huenda vikaongezeka na kufikia kiwango cha juu zaidi katika muda wa miaka 40.
Ugonjwa wa kifaduro ni maambukizo ya bakteria yanayoathiri mapafu na mfumo wa kupumua na huathiri watu wa rika zote ingawa watoto wachanga na wazee ndio walioko kwenye hatari zaidi.