1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa kuongeza kasi kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

22 Novemba 2025

Rasimu ya makubaliano ya mkutano wa mabadiliko ya tabianchi wa COP 30 imeonesha kuwa mataifa yamekubaliana kuhusu hatua za kusaidia kuongeza kasi ya kuchukua hatua dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.

Brasilien Belém 2025 | COP30-Klimagipfel
Mkutano wa tabianchi Brazil Novemba 2025Picha: Judit Alonso Gonzalbez/DW

Imebainisha pia makubaliano kuhusu kutathmini vikwazo vya kibiashara na kuongeza fedha kwa mataifa yanayoendelea ili kuyasaidia kukabiliana na ya hali mbaya ya hewa.

Miongozo kuhusu nishati ya visukuku kutolewa

Rais wa Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi COP30 Correa do Lago amesema taasisi yake itachapisha miongozo juu ya nishati ya visukuku na misitu na kwamba hakuna makubaliano yaliyofikiwa kuhusu masuala hayo. Awali mkutano huo ulikabiliwa na mkwamo kutokana na mataifa kutofautiana kuhusu suala la kutaja nishati ya visukuku katika azimio la mwisho la pamoja.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW