Israel yakasirishwa na matamshi ya Waziri Mkuu wa Uhispania
30 Novemba 2023Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema alimuagiza waziri wake wa mambo ya nje, Eli Cohen, kumwita balozi wa Uhispania ili kutoa karipio "baada ya kauli ya aibu ya waziri mkuu wa Uhispania katika siku ambayo magaidi wa Hamas wanawaua Waisraeli katika mji mkuu wetu Jerusalem".
Wapiganaji wawili wa kundi la Hamas waliwauwa raia watatu katika kituo cha mabasi cha Jerusalem wakati wa asubuhi siku ya Alhamisi.
Soma pia: Israel na Hamas waendelea kubadilishana mateka na wafungwa
Kundi lhilo la Palestina lina ngome yake katika Ukanda wa Gaza, ambako lilianzisha mashambulio ya Oktoba 7 nchini Israel, na kusababisha vita.
Katika chapisho la mtandao wa kijamii, Cohen alisema balozi wa Israel nchini Uhispania alikuwa ameitwa nyumbani kwa mashauriano.
"Israel inajiendesha na itaendelea kujiendesha kwa mujibu wa sheria za kimataifa," Cohen alisema.