1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matarajio ya mkutano wa G20 mjini London.

Sekione Kitojo1 Aprili 2009

Mkutano wa kundi la mataifa ya G20 unaanza leo mjini London. Nini matarajio yake ya kufikiwa mfumo imara wa fedha duniani?

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, kulia, akizungumza na waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier.Picha: AP


Miezi minne na nusu baada ya mkutano wa kifedha duniani mjini Washington , mataifa yenye utajiri mkubwa wa viwanda duniani na mataifa yanayoinukia kiuchumi ya kundi la G20, yanakutana mjini London leo Aprili mbili kufikia makubaliano muhimu, ya kuimarisha mfumo wa fedha duniani. Katika mkutano huo viongozi wa mataifa hayo wanachotakiwa kufanya ni kuzuwia kutokea kwa mzozo kama huo wa kifedha , kama hali ilivyo hivi sasa duniani.

Tangu mwezi Novemba mwaka jana takriban kwa muda mrefu wamekuwa wakionekana waendesha majadiliano wa mataifa ya G20 wakisafiri huku na huko. Kulikuwa na orodha ndefu ya mambo ya kufanyia kazi. Mpango wa kuchukua hatua ambao ulifikiwa hapo Novemba 15 katika mkutano wa dunia wa kifedha mjini Washington, ambao unajumuisha vipengee 47. Inatosha kuwa na sheria bora na mtazamo wa kifedha wa dunia katika kupata utaratibu mpya wa malipo ya wakuu wa makampuni. Sehemu kubwa kwa hiyo, wanasema wanahistoria wengi waliokutana katika mji mkuu wa Marekani , kuwa ilibidi kupata ufumbuzi hadi kufika Machi mwaka huu. Hadi sasa kumekuwa na mikutano ya hapa na pale. Umoja wa Ulaya, umoja wa mataifa ama jumuiya ya mataifa ya kusini mashariki mwa Asia, kila mmoja anajaribu kutafuta jibu la tatizo hilo. Ni vipi mfumo wa fedha wa kimataifa unapaswa kuwa hapo baadaye.

Viwango viko wazi.

Tunakiri kuwa masoko yote ya fedha, bidhaa na washiriki, pamoja na fedha zinazotengwa kwa ajili ya wakati wa dharura, pamoja na mashirika ya walanguzi na wachuuzi wengine wa kibinafsi ni lazima wawekewe utaratibu. Taratibu za dharura ni lazima zichukuliwe na kuwa sehemu ya mpango huo wa kuchukua hatua.


Hayo ameyasema kansela wa Ujerumani Angela Merkel baada ya mkutano wa mataifa ya Ulaya mwishoni mwa mwezi wa Februari. Nae Jean-Calude Trichet mkuu wa benki ya Ulaya ameeleza wazi kuwa , kila kitu lazima kibadilike. Lakini mzozo huu wa sasa wa kiuchumi unaonyesha kuwa mfumo mzima umeharibika na hauko madhubuti vya kutosha.

Suala kuu liko katika mpango huo wa utekelezaji. Kuimarisha hali ya uwazi na kuimarisha uchunguzi katika masoko ya fedha. Kuwa na mtazamo imara na uendeshaji bora wa masoko.

Kwa hivi sasa Uingereza na Marekani tayari zimekwisha onja joto la jiwe. Kwa kuwa hapo zamani mataifa hayo yamekuwa yakitabasamu tu , wakati wengine wakilizungumzia suala la mfumo hatari uliochoka wa kibepari. Lakini hivi leo waziri wa fedha wa Marekani Timothy Geithner anaonekana nae kama anachukua mtazamo kama huo.

Hatari kama hizi hazijali mipaka ya nchi. Tunalazimika kuchukua mtazamo thabiti na kupata sheria za wazi kwa ajili ya mfumo wa fedha wa kimataifa. Haya yatakuwa madai makuu ya kitaifa na kimataifa.


Shirika la fedha la kimataifa linapaswa kuchukua jukumu kubwa zaidi la uongozi katika mzozo huu na kiasi cha dola bilioni 500 zimetengwa, ili kupambana na mzozo huu, kwa mfano katika kutoa mikopo ya dharura kwa nchi mbali mbali zilizomo katika matatizo.

►◄

Author Böhme Henrik /ZR

Sekione Kitojo.



Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW