Matarajio ya Wakenya baada ya ziara ya Koffi Annan nchini humo
9 Oktoba 2009Matangazo
Mashirika yasiyo ya kiserikali yanasema linalohitajika ni Annan kubuni jopo la uchunguzi litakaloyashirikisha mashirika ya kiraia na viongozi wa dini, ili wawasukume viongozi wawajibike kuharakisha hatua za mageuzi, la sivyo ziara za Annan zitakuwa ni za bure. Munira Muhammad alizungumza na Cyprian Nyamwamu, mkurugenzi wa shirika la National Convention Executive Council, mwavuli wa asasi za kiraia nchini Kenya. Alianza kwa kumuuliza Iwapo viongozi wa kisiasa nchini Kenya wanamheshimu Annan, Wakenya watarajie nini kutoka kwa Rais Kibaki na Waziri mkuu Raila Odinga.
Mwandishi: Munira Muhammad.
Mhariri:Hamidou Oummilkheir