1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matayarisho ya Kombe la Dunia yakamilika

Michael Kwena
10 Juni 2026

Matayarisho ya michuano ya kombe la Dunia la 2026 yamekamilika huku jumla ya mataifa 48 yakitarajiwa kushiriki kipute hicho kinachoandaliwa kwenye mataifa ya Marekani,Canada na Mexico kuanzia kesho Alhamisi.

Kanada Vancouver 2026 | Science World als FIFA-WM-Spielball verkleidet
Maandalizi kuelekea mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA yakamilikaPicha: Jennifer Gauthier/REUTERS

Baada ya kipindi kirefu cha matarayisho, hatimaye mbivu na mbichi zitaanza kujulikana wakati jumla ya timu 48 zitakapoanza kushuka dimbani kuanzia kesho. Mechi ya ufunguzi itakuwa ya wenyeji Mexico wakiwavaa waakilishi wa bara la afrika,Afrika Kusini kwenye mchezo wa Kundi A. Kundi hilo pia linajumuisha, Korea Kusini na Jamhuri ya Czech.

Mechi hizi zinaandaliwa baada ya misururu ya mechi za kirafiriki ambapo timu kutoka Afrika zimekuwa zikipimana nguvu na kunoa makali yao kabla ya kipute cha kombe la Dunia kuanza rasmi.Katika mchezo wa kirafiki wa jana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilipigwa magoli 2 kwa moja na timu ya taifa ya Chile.

Lakini michuano ya mwaka huu, inafanyika wakati migogoro na majanga yakiendelea duniani ikiwemo mzozo wa Mashariki ya Kati na janga la Ebola.

Wachezaji wakipigania mpira wa kichwa wakati wa mechi ya fainali ya mchujo wa Kombe la Dunia kati ya Iraq na Bolivia mjini Monterrey, MexicoPicha: Fernando Llano/AP Photo/picture alliance

Ukaguzi wa wachezaji umekuwa ukifanyika, ambapo tukio la hivi punde lilikuwa kukaguliwa kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Senegal nchini Marekani kabla ya mechi yao ya kirafiki.  Video ziliwaonyesha wachezaji hao wakikaguliwa kwa kina mmoja baada ya mwingine baada ya kushuka kutoka kwenye ndege.

Hata hivyo, Shirikisho la Soka la Senegal limefafanuwa kuwa, hiyo ilikuwa ni sehemu ya utaratibu wa kiusalama na kwamba, haikuwa ni maonevu kama ilivyoripotiwa.

Matukio haya yanajiri wakati licha ya kuwa na visa na mwaliko kutoka shirikisho la soka duniani FIFA.

Omar amewaambia waandishi wa habari mjini Mogadishu baada ya kuwasili kwamba, kilichotokea dhidi yake nchini Marekani hakipaswi kuwavunja moyo vijana kutoka taifa hilo.

Shangwe Mogadishu baada ya mwamuzi Artan kurudi nyumbani

01:10

This browser does not support the video element.

Afrika inawakilishwa na timu 10 zikiwemo,Morocco, Senegal, Ivory Coast, Algeria, Kongo, Misri, Afrika Kusini, Ghana, Cape Verde na Tunisia.

Likizo Mexico kwaajili ya ufunguzi wa kombe la dunia

Kama sehemu ya maandalizi ya michuano hiyo, mamlaka nchini Mexico imewaagiza wanafunzi kusalia nyumbani kesho huku watumishi wa umma, wakitakiwa kufanya kazi nyumbani ili kuepusha msongamano mkubwa wa magari wakati michuano hiyo itakapong'oa nanga katika Uwanja wa Azteca.

Rais Claudia Sheinbaum ametia saini agizo hilo huku Madaktari, maafisa wa polisi na wafanyakazi wa miundombinu muhimu wakitakiwa kuendelea na kazi kama kawaida.

Rais wa FIFA Gianni Infantino akiwa ameshika kombe la Kombe la DuniaPicha: Raymond Carlin III/IMAGN Images/REUTERS

Matiafa mbalimbali yako tayari katika michuano hiyo huku mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi akishiriki michezo hiyo kwa mara ya sita. Katika mchezo wao wa kirafiki Argentina iliwapiga Iceland magoli 3 kwa bila, Messi akifunga kupitia mkwaju wa penalti.

Kwingineko, Mshambuliaji Nick Woltemade wa timu ya taifa ya Ujerumani, amesema anajihisi yuko tayari kushiriki Kombe la Dunia, licha ya kupitia msimu wake wa kwanza wenye changamoto katika klabu ya Newcastle United inayoshiriki Ligi Kuu ya uingereza.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alianza vyema msimu wake kwa kufunga mabao saba katika nusu ya kwanza ya msimu. Hata hivyo, tangu mwezi Januari, alifanikiwa kuongeza bao moja pekee, jambo lililozua mjadala na ukosoaji mkubwa kutoka kwa wachambuzi na mashabiki.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW