Mateka mmoja wa Kijerumani yuhai
22 Julai 2007Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier,alipozungumza na waandishi wa habari mjini Berlin alisema:
“Sasa kilichokuwepo ni kujitahidi kuchukua kila hatua inayowezekana kibinadamu na inayowajibika, ili kuokoa maisha ya mateka wa pili.“
Hapo awali,msemaji wa Taliban alidai kuwa kundi hilo la wanamgambo limewauawa mateka wote wawili. Wahandisi wawili wa Kijerumani na wafanyakazi wenzao watano wa Afghanistan,walitekwa nyara katikati ya Afghanistan,walipokuwa wakifanya kazi katika mradi mmoja wa bwawa.