1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mateka wa kike wa Colombia waachwa huru

11 Januari 2008

---

CARACAS

Mateka wawili wanawake waliokuwa wakishikiliwa na waasi wa kimaxisti nchini Colombia wamemshukuru rais Hugo Chavez kwa jitihada zake zilizofanikisha kuachiwa kwao.Rais Chavez alizungumza hapo jana kwa njia ya simu na mabibi Consuelo Gonzalez na Clara Rojas waliochukuliwa kutoka msitu mkubwa wa Colombia na helikopta za Venezuela.Wanawake hao walionekana kuwa katika hali nzuri na furaha walipowasili katika kambi ya kijeshi ya Venezuela baada ya kuzuiliwa mateka kwa miaka sita na waasi wa kundi la FARC.Wanawake hao mashuhuri nchini Colombia wamemtolea mwito rais Chavez kusaidia katika kuwakomboa mateka wengine kiasi cha 40 wanaoendelea kuzuiliwa na waasi akiwemo mwanasiasa Ingrid Betancourt ambaye ni bosi wa zamani wa bibi Rojas.