1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mateka wanaoshikilia na FARC bado kuachiliwa Colombia

31 Desemba 2007

BOGOTA

Kukabidiwa kunakosubiriwa kwa hamu kwa mateka watatu wanaoshikiliwa na waasi wa sera za mrengo wa shoto nchini Colombia kunaweza kuchukuwa siku mbili tatu zaidi.

Kundi la waasi la FARC nchini Colombia hadi sasa limeshindwa kutaja mahala pa siri vichakani ambapo mateka hao walikuwa waachiliwe juu ya kwamba kumekuwepo na uvumi kwamba mjumbe wa Venezuela katika mchakato huo tayari amejulishwa juu ya mahala hapo.

Rais Hugo Chavez wa Venezuela amekuwa akishughulikia mchakato wa kuachiliwa kwa mateka hao kama sehemu ya jaribio la kuachiliwa kwa mateka wote wanaoshikiliwa kwa miaka mingi na kundi hilo la FARC.

Awali kuachilikwa kwa mateka hao kulitazamiwa kufanyike hapo Ijumaa.