1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Mateka watatu walioachiliwa na Hamas wana afya njema

20 Januari 2025

Madaktari nchini Israel wamesema mateka watatu walioachiliwa na kundi la Hamas kama sehemu ya awali ya makubaliano ya mabadilishano wapo katika hali nzuri ya kiafya na tayari mateka hao wameungana na familia zao.

Israel, Ramat Gan | Romi Gonen
Baadhi ya mateka wa israel walioachiliwa na Hamas wakikumbatiana na jamaa zao kwenye kituo cha afya cha Ramat Gan, IsraelPicha: Maayan Toaf/GPO/Handout/REUTERS

Emily Damari, Romi Gonen na Doron Steinbrecher ambao walitekwa wakati wa shambulio la oktoba saba mwaka 2023 waliachiliwa hapo jana Jumapili baada ya kushikiliwa na Hamas kwa zaidi ya miezi 15 katika Ukanda wa Gaza.

Israel kwa upande wake imewaachilia wafungwa 90 wa Kipalestina leo Jumatatu. Msemaji wa Hamas amethibitisha kuwa mateka wanne wa Israel wataachiliwa siku ya Jumamosi ijayo kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana mateka 33 kwa wafungwa 1,904 wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel katika kipindi hicho ya wiki sita.

Katika hatua nyingine wapalestina wameanza kurejea katika makazi yao huko Gaza baada ya kusitishwa kwa mapigano ingawa wengi wanaeleza kwamba makazi yao yameharibiwa vibaya. Huyu ni Ahmed Al Akhrasa akisimulia jinsi alivyoyakuta makazi yake.

Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na wapatanishi ambao ni Marekani, Qatar na Misri.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW