1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Mateka wengine 13 wanaoshikiliwa na Hamas kuachiwa huru

26 Novemba 2023

Mateka wengine 13 wanaoshikiliwa na kundi la wanamgambo la Hamas wanatarajiwa kuachiwa huru leo ikiwa ni siku ya tatu ya makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano kati ya kundi hilo na Israel katika ukanda wa Gaza

Mfungwa wa Palestina arejea Jerusalem baada ya kuachiwa huru kutoka gereza la Israel mnamo Novemba 24,2023
Mfungwa wa Palestina arejea Jerusalem baada ya kuachiwa huru kutoka gereza la IsraelPicha: Muammar Awad/Xinhua/picture alliance

Kundi la Hamas limewasilisha kwa Israel orodha ya majina 13 ya mateka wanaopaswa kuachiwa huru Jumapili ( 26-11-2023) huku baadhi ya raia wa Marekani wakiwa miongoni mwa kundi hilo la mateka. Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu imethibitisha mapema leo kwamba imepokea orodha ya majina zaidi ya mateka watakaoachiwa, ingawa haikutaja idadi iliyotolewa.

Kundi la pili la mateka liliachiliwa huru Jumamosi ( 25-11-2023)

Kundi la pili la mateka 17 waliachiliwa huru jana jioni. Kwa upande wake, Israel iliwaachia huru wafungwa 39 wa Kipalestina kutoka magerezani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW