1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo ya kwanza ya kura ya rais Marekani yatangazwa

5 Novemba 2024

Matokeo ya kwanza ya uchaguzi wa Marekani yametangazwa katika kijiji kidogo cha Dixville Notch huko New Hampshire ambapo wagombea wote wawili wa urais Kamala Harris na Donald Trump wamefungana kikura.

Uchaguzi Mkuu Marekani 2024 | Wananchi wakipiga kura
Baadhi ya Wamarekani wakipiga kuraPicha: Nathan Posner/Anadolu/picture alliance

Mgombea wa Democratic Harris amepata kura 3 sawa na mwenzake wa Republican Trump.

Matokeo hayo yametangazwa muda mfupi baada ya saa sita usiku wa kuamkia leo.

Kijiji hicho kilicho karibu na mpaka wa Canada kimeshuhudia vituo vya kupigia kura kufunguliwa saa sita usiku.

Kijiji cha Dixville Notch kimekuwa na utamaduni huo wa kufungua vituo vya upigaji kura usiku tangu mwaka 1960.

Soma pia:Uchaguzi wa Marekani: Nini kinatokea siku ya uchaguzi na baadae?

Kwa kuwa wapiga kura waliojiandikisha ni sita pekee, zoezi la kuzihesabu kura hizo linafanyika kwa haraka.

Televisheni nchini Marekani zilirusha moja kwa moja zoezi hilo la upigaji kura na kuhesabiwa kwake.