1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Tinubi aongoza katika matokeo ya mwanzo ya uchaguzi Nigeria

28 Februari 2023

Matokeo ya mwanzo katika uchaguzi wa Nigeria uliofanyika mwishoni mwa wiki yanaonesha Bola Tinubu wa chama tawala akiwa kileleni. Hayo ni kwa mujibu wa hesabu za shirika la habari la Reuters katika majimbo 25 kati ya 36

Nigeria Wahlen 2023/Präsidentschaftskandidat Bola Ahmed Tinubu
Picha: Emmanuel Osodi/AP Photo/picture alliance

Matokeo ya tume ya uchaguzi kutoka majimbo hayo yanaonesha Tinubu wa chama cha All Progressives Congress, APC, akiwa mbele na karibu asilimia 36 au milioni 7 ya kura halali zilizohesabiwa, naye Atiku Abubakar wa chama kikuu cha upinzani, Peoples Democratic, PDP, akimfuata kwa karibu na asilimia 30 au karibu milioni 6 ya kura halali.

Peter Obi wa chama kidogo cha Labour ana asilimia 20 au karibu milioni 3.8. Matokeo zaidi yanatarajiwa kumuonyesha mshindi baadaye leo. Vyama vya upinzani vinapinga matokeo hayo vikisema yalitokana na mchakato uliokumbwa na udanganyifu ikiwemo matatizo ya kiufundi kutokana na mfumo mpya wa teknolojia ulioletwa na tume ya uchaguzi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW