1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo ya Uchaguzi Bavaria ni pigo kwa CSU

Oumilkheir Hamidou
15 Oktoba 2018

CSU yapoteza kura, sawa na SPD huku walinzi wa mazingira die Grüne wakishinda maradufu na AfD kuwakilisha bungeni. Pigo hilo dhidi ya CSU ni kubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa tangu kilipoundwa miaka zaidi ya 60 iliyopita.

Deutschland Reaktionen auf Bayern Wahl Angela Merkel in Berlin
Picha: Getty Images/AFP/J. Macdougall

Katika uchaguzi wa bunge la jimbo la kusini la Bavaria, chama cha Christian Social Union-CSU kimepata pigo kubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa tangu kilipoundwa miaka zaidi ya 60 iliyopita. Wa kulaumiwa zaidi ni Horst Seehofer. Na pigo hilo litaathiri pia siasa za serikali kuu mjini Berlin, anasema Rosalia Romaniec katika uhariri wake.

Uchaguzi huo utabadilisha mengi. Na sio tuu katika jimbo la Bavaria. Mafanikio ya miongo kadhaa iliyopita, ya chama cha Christrian Social Union-CSU, kilichokuwa kikiaminika na kupendwa na wapiga kura kama chama kinachofuata mwongozo wa Kikristo, kihafidhina na wakati huo huo kijamaa, imani hiyo sasa imetoweka. Kutoka takriban assili mia 48 ya kura kimeporomoka hadi asili mia 37- ni pigo kubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa.

Kimoja lakini ni dhahir: pigo la chama hicho kikubwa kabisa katika jimbo la Bavaria halijatokana na ufanisi wa wengine. Wakubebeshwa jukumu la zilzala hiyo ni viongozi wenyewe wa chama hicho.

Maajabu makubwa zaidi katika uchaguzi huo ni ushindi wa walinzi wa mazingira-die Grüne. Wakijikingia karibu asaili mia 19 ya kura wamezidisha mara dufu idadi ya kura na wanafuata njia ya kutangazwa chama cha umma, mpaka katika daraja ya taifa.

Chama cha die Grüne chapata kura zaidi

Katika jimbo la Bavaria, wapiga kura wengi wa CSU wamekipigia kura chama cha die Grüne, wanahisi wanathamini zaidi Ukristo kuliko wao. Na hasa kiongozi wa CSU, Horst Seehofer anaonyesha kusahau maadili ya Kikristo. Lakini zaidi kuliko yote wapiga kura hawakutaka tena kudanganywa eti hofu dhidi ya kuenea Uislam ni kubwa kuliko busara na kupendana.

Miongoni mwa vyama ndugu ,CSU ndio wanaoangaliwa kama nguzo ya siasa za kihafidhina.Picha: Getty Images/AFP/O. Andersen

Mshindi mwengine ni wa wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia AfD. Watawakilishwa katika bunge la 15 kati ya 16 ya majimbo ya Ujerumani. Kwamba hawakupata kama ilivyokuwa ikihofiwa asili mia 20, badala yake wamejikusanyia asili mia  10 "tu" ni mbaya ingawa hatuwezi kusema Bavaria inaelemea mrengo wa kulia. Ni matokeo ya kura ya malalamiko na makosa ya CSU.

Kosa kubwa zaidi ni kuvunja miko kuelekea mrengo wa kulia. Kwa miongo kadhaa chama hicho cha Bavaria kimekuwa kikifuata nyayo za kiongozi wake shupavu Franz-Josef Strauß .Ilikuwa muhimu mpaka katika daraja ya shirikisho: miongoni mwa vyama ndugu ,CSU ndio wanaoangaliwa kama nguzo ya siasa za kihafidhina.

CSU yaiga AfD?

Hali hiyo iliwezekana kwa miongo kadhaa hadi mwaka 2018, uongozi wa chama hicho cha Bavaria ulipoingiwa na wahka na kuanza kuigiza siasa ya AfD. Makosa yalipodhihirika, mwenyekiti wake, mpinzani mkubwa wa kansela Merkel alikuwa tayari ameshavuruga mengi tu. Horst Seehofer umeula na chua, wewe ndie chanzo na wewe pia ndie iliyeshindwa.

Madhara ya  tamaa ya Seehofer yanasababisha mmomonyoko wa vyama ndugu,bila ya kuitaja zahma inayopiga dhidi ya SPD.

Wajerumani saasa wanaelekeza macho yao Hessen ambako uchaguizi wa jimbo utaitishwa wiki mbili kutoka sasa.Unaweza kugeuka uchaguzi utakaoamua hatima ya serikali kuu ya muungano mjini Berlin.

Mwandishi: Romaniec, Rosalia/ Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Mohammed Khelef

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW