1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo ya uchaguzi Kenya kutangazwa saa tisa

Wakio Mbogho15 Agosti 2022

Matokeo ya uchaguzi wa Rais nchini Kenya ambayo yamekuwa yakisubiriwa kwa siku sita sasa yanakaribiwa kutangazwa. Tume ya Uchaguzi tayari imejumlisha zaidi ya asilimia 80 ya matokeo ya majimbo yote 290.

Kenia Wahlen 2022
Picha: Yasuyoshi Chiba/AFP

Kulingana na katiba ya Kenya, matokeo lazima yatolewe ifikapo kesho Jumanne. Matokeo ya awali ya Tume ya Uchaguzi, IEBC, yanaonesha Naibu Rais, William Ruto, anaongoza kwa idadi ndogo ya kura dhidi ya mwanasiasa wa muda mrefu na mpinzani wake mkuu, Raila Odinga. 

IEBC imekuwa ikikabiliwa na ukosoaji mkali wa jinsi ilivyoshughulikia uchaguzi wa Agosti mwaka 2017, ambao katika historia ya kwanza barani Afrika ulibatilishwa na Mahakama ya Juu baada ya Odinga kupinga matokeo hayo. Mamia ya watu waliuawa katika machafuko yaliyofuatia uchaguzi huo, huku ukatili wa polisi ukilaumiwa kwa vifo hivyo.

Matokeo ya Nakuru

Picha: Sayyid Abdul mAzim/AP/picture alliance

Tume ya uchaguzi ya Kenya ililazimika kuhamisha kituo cha ujumlishaji wa kura cha kaunti ya Narok kutoka chuo kikuu cha Maasai Mara hadi Jumba la Bomas jijini Nairobi kutokana na vurugu iliyogubika zoezi la kuhesabu kura za wagombea wa ugavana wa kaunti hiyo. Moitalel Ole Kenta kutoka muungano wa Azimio la Umoja one Kenya alidai kuna wizi ulikuwa unaendelea.

Licha ya juhudi zake kutaka kusimamisha zoezi la kuhesabu kura, shughuli hiyo iliendelea na mshindi kupatikana. Baada ya Subira ya siku tano, IEBC ilimtangaza Patrick Ole Ntutu wa chama cha UDA kama gavana wa kaunti ya Narok akimpiku mpinzani wake. Ole Ntutu ametumia ukurusa wake wa mtandao wa kijamii kuwashukuru wafuasi wake kwa kumpigia kura akiahidi kuyaangazia maslahi yao katika utawala wake.

Ngome ya Odinga ?

Polisi wanawalaumu wagombea hao wa ugavana kwa vurugu na taharuki iliyoshuhudiwa eneo la Narok tangia zoezi la ujumlishaji wa kura kuanza. Wanawazuia baadhi ya watu waliokamatwa kwenye vurugu hiyo wakiwemo maafisa wa uchaguzi ili kuwasaidia katika uchunguzi zaidi. Kamishna wa kaunti ay Narok Isaac Masinde anael

Kaunti ya Narok ipo kwenye eneo la bonde la ufa na kwa muda mrefu limetambulika kama ngome ya kiongozi wa Azimio la Umoja one Kenya Raila Odinga kutokana na ushawishi wake mkubwa eneo hilo. Lakini kwenye kampeini za uchaguzi huu mkuu Naibu Rais Wiliam Ruto aliweka juhudi kulivutia eneo hilo hata kulizuru mara kwa mara.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW