1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo ya uchaguzi Kongo

20 Agosti 2006

TAARIFA YA HABARI 20-08-06 12.00

KINSHASA:

Wakuu wa Tume ya uchaguzi katika jamhuri ya kidemokrasi ya kongo wanatazamiwa kutangaza leo matokeo ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa mwezi uliopita na wa bunge.Tume huru ya uchaguzi imebainisha kwamba, rais wa sasa Joseph Kabila ameshindwa kujipatia zaidi ya nusu ya kura-50% .Hii ina maana ,uchaguzi wa rais utaingia duru ya pili hapo oktoba 29.Unatarajiwa kwahivyo kuwakumbanisha watetezio 2 uso kwa uso-rais Joseph Kabila dhidi ya makamo-rais Jean-Pierre Bemba,ambae kwa muujibu wa matokeo yasio-rasmi ndie aliemkaribia mno rais Kabila katika kura.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW