1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo ya uchaguzi ya hivi punde

27 Septemba 2009

Matokeo ya wakati huu ya uchaguzi wa Bunge la Ujerumani Bundestag yaliotoleawa na vituo vya televisheni vya ARD na ZDF yanaashiria wahafidhina wa vyama ndugu vya CDU na CSU vinavyoongozwa na Kansela Angela Merkel vimepata asili mia 33.6 ya Kura yakiwa matokeo ya pili mabaya katika enzi ya baada ya vita vya pili vya dunia.Katika uchaguzi uliopita 2005 vilinyakua asili mia 35.2 ya kura

Lakini FDP, kinachoongozwa na Guido Westerwelle ambacho kimeshuhudia uungaji wake mkono ukipanda kutokana na msukosuko wa fedha duniani,ulioiathiri pua Ujerumani, kiliutumia mwanya huo na kujinyakulia asili mia 14.6 ya kura, matokeo bora kabisa katika historia yake.

Chama cha SPD kilichokua mshirika na CDU katika serikali ya mseto kwa miaka minne iliopita, kimepata matokeo mabaya kabisa tangu vita vya pili vya dunia,kwa kupata asili mia 23.1 tu ya kura. Mgombea wake wa Ukansela Franz walter Stenmeier aliyekua Makamu wa Kansela na Waziri wa nje katika serikali ya mseto ilioongozwa na Bibi Merkel ameyaita matokeo hayo kuwa " machungu."

Matokeo pia yameashiria chama cha Kijani kimejikingia asili mia 10.2 ya kura , kikiachwa nyuma na kile cha mrengo wa shoto Linke, kilichowashangtaza wengi kwa kujipatia 12.1 asili mia ya kura.

Matokeo hayo yamevipa nafasi CDU/CSU na FDP kuunda serikali ijayo ya muungano na mhula wa pili kwa Bibi Angela Merkel kama Kansela. Kiongozi wa FDP Westerwelle anatarajiwa kuwa Waziri wa mambo ya nchi za nje na Makamu wa Kansela.

Mwandishi: M.Abdul-Rahman /Reuters

Mhariri: Sekione Kitojo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW