Chuki dhidi ya Wayahudi yameongezeka Ujerumani
28 Novemba 2023Kwa mujibu wa muungano wa idara za utafiti inayokusanya matukio ya chuki dhidi ya Wayahudi RIAS, ni kwamba Ujerumani inaripoti matukio ya chuki 29 kwa siku, idadi hiyo ikiwa zaidi ya asilimia 320 ya wastani wa kila siku ya rekodi zilizokusanywa mwaka 2022.
Utafiti huo ulifanyika katika ya Oktoba 7 hadi Novemba tarehe 9 mwaka huu. RIAS imeeleza kuwa Wayahudi wengi walikabiliwa na matukio ya chuki na kwamba maisha yao yako hatarini.
Soma pia:Ulaya yakabiliwa na ongezeko la chuki dhidi ya Wayahudi
Mjini Giessen kwa mfano, wanaume wawili waliingia kwenye nyumba na kuiondoa bendera ya Israel iliyokuwa inaning'inia nje ya dirisha.
Matukio ya chuki dhidi ya Wayahudi na propaganda dhidi ya Israel pia yameongezeka katika vyuo vikuu. Wanafunzi Wayahudi wameeleza kuwa, wanafunzi wenzao wamewalaumu kwa vitendo vinavyofanywa na serikali ya Israel huku wanafunzi wengine wakiacha kabisa masomo.