1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumaini mapya Zimbabwe

23 Desemba 2009

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na hasimu wake Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai wamekubaliana kuunda tume zitakazoshughulikia mageuzi katika sekta muhimu na hivyo kutoa matumaini mapya kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa.

ARCHIV - Robert Mugabe (Archivfoto vom 09.11.2008). Drei Monate hat es gedauert, bis Präsident Robert Mugabes Regierung Warnungen der Hilfsorganisationen ernst genommen und SOS gefunkt hat. Während seine Schergen weiter den mitunter aufkeimenden Widerstand niederknüppeln oder durch Einschüchterungen einzugrenzen versuchen, ufert die Not aus. Nun soll die Weltöffentlichkeit richten, was er bei seinem Ringen um die Macht billigend in Kauf genommen hat: den totalen Kollaps des einstigen Musterstaates. Foto: JON HRUSA (zu dpa-KORR "Simbabwes Kollaps mündet in einen verzweifelten Überlebenskampf") +++(c) dpa - Bildfunk+++
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe.Picha: picture-alliance/ dpa

Taarifa iliyotolewa kufuatia mkutano wa Jumatatu kati ya Rais Mugabe na Waziri Mkuu Tsvangirai imesema kuwa viongozi hao wamewateua wajumbe wa Halmashauri ya Vyombo vya Habari, Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe na Halmashauri ya Haki za Binadamu ya Zimbabwe. Halmashauri hizo mpya zinatazamiwa kuleta mageuzi yaliyo muhimu sana kuvutia misaada ya kigeni. Wadadisi wanasema, uamuzi wa kuunda tume hizo mpya unatia moyo. Lakini mchambuzi Barnabas Thondlana anatanguliza mbele ukweli wa hali ya mambo.Anasema:

"Tunachohitaji ni kuimarisha taasisi na sio mtu mmoja mmoja. Watu hao wanaweza kubadilishwa lakini taasisi baadae huenda zikaendelea kuwa na matatizo."

Licha ya kuteuliwa kwa wajumbe wa halmshauri hizo tatu mpya, bado kuna masuala mengine ya utata. Kwa mfano Mugabe anakataa kumuapisha Roy Bennet kama makamu wa waziri wa kilimo.Bennet ni mshirika mwandamizi wa Tsvangirai na anakabiliwa na mashtaka ya uhaini. Vile vile Mugabe anakataa kuwafukuza kazi washirika wake wawili aliewateua kuiongoza Benki Kuu na kushika wadhifa wa Mwanasheria Mkuu.

Katika mwezi wa Oktoba,Tsvangirai wa chama cha MDC alitangaza kuwa anajitoa katika serikali ya umoja wa kitaifa kwa sababu ya kutoweza kuafikiana kuhusu mada hizo. Chama cha ZANU-PF cha Mugabe kilipewa muda, hadi Januari 15 kuafikiana katika masuala hayo yote. Lakini majuma matatu baadae, Tsvangirai alirejea kufuatia jitahada za upatanishi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC- zilizoomgozwa na nchi jirani Afrika Kusini. Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini alieleza hivi:

Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai.Picha: picture-alliance/ dpa

"Lilikuwa suala gumu sana. Tulizungumza na ndugu zetu wa Zimbabwe. Nadhani wameashiria kuwa wapo tayari kuhakikisha kuwa makubaliano yao yatatekelezwa. Kwa maoni yangu, sote tunapaswa kuwaunga mkono."

Makubaliano yaliyopatikana juma hili kati ya mahasimu Mugabe na Tsvangirai huenda ikawa ni hatua ndogo ya kwanza inayotoa matumaini kuwa serikali ya umoja wa kitaifa itadumu licha ya Rais Mugabe hivi karibuni tu kutamka kuwa serikali hiyo haina muda mrefu hivyo.

Mwandishi:Genthe,Jana/ZPR/P.Martin/RTRE

Mhariri: Miraji,Othman