MATUMAINIO YA AMANI-SUDAN:
7 Desemba 2003Matangazo
NAIVASHA: Matumainio ya kupatikana amani ya kudumu nchini Sudan yameongezeka baada ya Naibu rais wa Sudan Ali Osman Taha na John Garang kiongozi wa kundi la waasi wa kusini-SPLA, kuwasili kwa majadiliano nchini Kenya.Kwa mujibu wa Taha,mazungumzo yaliofanywa hapo awali yamefungua njia ya kile alichokiita,"makubaliano ya mwisho".Waziri wa kigeni wa Sudan,Mustafa Ismail amesema makubaliano hayo yatatiwa saini mwisho wa mwaka huu.Hata wajumbe wa SPLA wamesema kuwa wana matumainio mazuri.Ismail akaeleza kuwa lengo la mazungumzo ya mjini Naivasha ni kupata suluhusho kwa masuala matatu yaliobakia:ugawaji wa madaraka,utajiri wa nchi,na hatima ya maeneo matatu yanayogombewa.Kwa wakati huo huo,afisa mmoja wa Kimarekani amesema Marekani ipo tayari kutoa msaada wa Dola milioni 200 kwa eneo la kusini la Sudan,lililo katika hali ya umasikini mkubwa-eneo ambalo lina utajiri wa mafuta.
