1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumizi ya kijeshi yaongezeka duniani-SIPRI

25 Aprili 2022

Ripoti ya SIPRI inasema bajeti za matumizi ya kijeshi barani Ulaya na Urusi ziliongezeka kabla ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine,licha ya kushuhudiwa athari za janga la Corona katika uchumi.

US-Panzer Symbolbild Waffenhandel
Picha: Andreea Alexandru/AP/dpa/picture alliance

Taasisi ya kimataifa ya utafiti kuhusu masuala ya amani duniani,iliyoko mjini Stolkholm Sweden imetoa ripoti yake ya mwaka ambayo inasema bajeti za matumizi ya kijeshi barani Ulaya na Urusi ziliongezeka kabla ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine,licha ya kushuhudiwa athari za janga la Corona katika uchumi.

Ripoti ya SIPRI imechapishwa leo Jumatatu na imeonesha kwamba katika kipindi kuelekea uvamizi wa Urusi nchini Ukraine matumizi ya kijeshi barani Ulaya na Urusi yaliongezeka.

Soma zaidi:Ripoti ya SIPRI- matumizi ya kijeshi yaongezeka duniani

Inasema vita nchini Ukraine ambavyo Urusi inaviita ni operesheni maalum ya kijeshi vimeilazimisha Ulaya kutafakari tena kwa haraka kuhusu mikakati yake ya ulinzi na kupelekea  nchi kadhaa kutoa ahadi ya kuongeza kwa kiasi kikubwa bajeti zao za kijeshi.

Lakini pia ni vita vilivyofungua njia ya uwezekano wa kutanuliwa kwa jumuiya ya kujihami ya NATO kuzijumuisha nchi za Finland na Sweden.

Na kwa namna inavyonesha ni kwamba athari kubwa kabisa za kuongezeka bajeti za kijeshi huenda zikaonekana waziwazi katika miaka inayokuja ingawa matumizi hayo ya kijeshi yalianza kuongezeka tangu mwaka 2021kutokana na ongezeko la mivutanokuelekea uvamizi huu wa Urusi unaoshuhudiwa sasa huko Ukraine.

Matumizi ya kijeshi duniani inaelezwa yalifikia dola Trilioni 2 kwa mara ya kwanza mnamo mwaka jana, ikiwa ni ongezeko la dola zinazofikia bilioni 2,113 ambazo ni asilimia 0.7 kutoka mwaka 2020.

Askari jeshi akiwa katika oparesheni ya kijeshiPicha: DW

Soma zaidi:Ripoti ya SIPRI: Watengenezaji wa silaha wakubwa duniani

Ongezeko hilo la bajeti za kijeshi linashuhudiwa kwa mwaka wa saba mfululizo kwa mujibu wa SIPRI ambayo ni taasisi yenye ushawishi mkubwa kuhusu masuala ya ulinzi duniani. Taasisi hiyo imebaini kwamba Urusi ni miongoni mwa nchi zilizoongoza duniani. Dokta Lopes da Silva ni mtafiti mwandamizi wa SIPRI.

''Mwaka 2021 Urusi iliongeza matumizi yake ya kijeshi kwa mwaka wa tatu mfululizo. Ongezeko hilo lilikuwa la asilimia 2.9 ambapo ilikuwa na bajeti ya dola bilioni 64.9 na ni nchi ya tano iliyokuwa na bajeti kubwa ya kijeshi duniani.''

Urusi imetajwa kutanguliwa na Marekani,China,India na Uingereza.

Mkurugenzi wa SIPRI anayehusika na mpango unaosimamia masuala ya matumizi ya kijeshi na utengenezaji silaha, Lucie Beraud-Sudreau amesema mapato makubwa yanayotokana na mafuta na gesi yameisaidia sana Urusi kujiimarisha kwani ilitumia dola bilioni 5.9 kwa matumizi ya kijeshi mnamo mwaka 2021 kwa mujibu wa SIPRI na bara la Ulaya kwa ujumla limetumia dola bilioni 418 katika matumizi yake ya kijeshi na bajeti hiyo imeongezeka kwa kasi tangu Urusi ilipolinyakua jimbo la Crimea mnamo mwaka 2014.

Kutoka mwaka 2020 bajeti ya masuala ya ulinzi imeongezeka kwa asilimia 3.0 na kubakia kuwa kubwa kwa asilimia 19 ikilinganishwa na hali ilivyokuwa mnamo mwaka 2012.

Soma zaidi:Matumizi ya kijeshi yapungua duniani

Ripoti ya SIPRI imebaini kwamba mifumo ya ulinzi wa makombora, ndege zisizoendeshwa na rubani na madege ya kivita ya kisasa hasa ndizo zana zilizonunuliwa na nchi nyingi zinazotajwa kutiwa hofu na Urusi.

Matumizi ya Kijeshi yaliongezeka 2017 -SIPRI

01:22

This browser does not support the video element.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW