1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauaji mengine Somalia

7 Juni 2005

Mogadishu:

Kiasi ya watu 16 wameuwawa na 8 kujeruhiwa katika mapigano tafauti katika miji miwili ya kaskazini mwa Somalia. Kiasi ya watu 11 waliuwawa katika kijiji cha Balli Guled kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu, na wengine watano wakauwawa katika mapigano makali ya makundi yanayohasimiana huko Beletweyne. Wadadisi wanasema kuendelea hali ya usalama kuwa mbaya nchini humo, kunazidi kuchelewesha mpango wa kurejea nyumbani kwa serikali ya mpito na bunge, vyombo ambavyo vingali bado katika mji mkuu wa Kenya-Nairobi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW