1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauaji ya ''El Mencho'' yazusha taharuki Mexico

23 Februari 2026

Machafuko ya mtandao wa kihalifu wa Jalisco New generation'' yamesababisha shughuli nyingi kusimama nchini Mexico

Kiongozi wa mtandao wa ulanguzi wa mihadarati Nemesio Oseguera Cervantes , maarufu kama ''El Mencho'' aliuwawa na jeshi la Mexico
Kiongozi wa mtandao wa ulanguzi wa mihadarati Nemesio Oseguera Cervantes , maarufu kama ''El Mencho'' aliuwawa na jeshi la MexicoPicha: US State Department/Anadolu/picture alliance

Hali ya wasiwasi imeongezeka nchini Mexico,shule zimefungwa katika majimbo mengi ya nchi hiyo wakati serikali na mataifa ya kigeni wakitowa tahadhari kwa raia wao kubakia majumbani.

Wasiwasi huo umesababishwa na machafuko yaliyozuka kufuatia kuuwawa kwa kiongozi wa mtandao wenye nguvu wa uhalifu unaofahamika kama ''Jalisco New Generation''.

Nemesio Ruben Osequera Cervantes kwa jina maarufu ''El Mencho'' aliyeuwawa na wanajeshi alikuwa kiongozi wa kundi hilo linalotajwa kukuwa kwa kasi  na ambalo limekuwa likihusika na kupeleka mihadarati nchini Marekani.Trump yuko tayari kuzungumza na maduro kuhusu magenge ya walanguzi Mexico

Ikulu ya Marekani imethibitisha kwamba nchi hiyo imetowa msaada wa kiintelijensia uliofanikisha operesheni hiyo ya kukamatwa El Mencho. Rais  Claudia Sheinbaum ametowa wito wa utulivu nchini humo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW