1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
HistoriaAfrika

Mauaji ya kwanza ya kimbari katika karne ya 20

21 Desemba 2023

Kati ya mwaka 1904 na 1908, wakoloni wa Kijerumani walifanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa jamii za Herero na Nama nchini Namibia, ukatili unaoendelea kujadiliwa hadi leo nchini humo.

Mfululizo wa Makala za Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani zinatayarishwa na DW, shirika la kimataifa la utangazaji la Ujerumani kwa ufadhili wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani (AA). Ushauri wa mambo ya historia umetolewa na Profesa Lily Mafela, Profesa Kwame Osei Kwarteng na Reginald Kirey.
Mfululizo wa Makala za Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani zinatayarishwa na DW, shirika la kimataifa la utangazaji la Ujerumani kwa ufadhili wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani (AA). Ushauri wa mambo ya historia umetolewa na Profesa Lily Mafela, Profesa Kwame Osei Kwarteng na Reginald Kirey.Picha: Comic Republic

Vipi Waherero na Wajerumani walikutana? 

Baada ya mipaka ya Ujerumani ya Afrika Kusini Magharibi kuanzishwa mwaka 1890, mamlaka za Ujerumani zililipadisha hadhi eneo hilo na kuwa koloni la walowezi, kinyume na miliki zake nyengine barani Afrika.

Soma zaidi: Uporaji wa ardhi: Kuzaliwa kwa Himaya ya Ukoloni wa Ujerumani

Walowezi walianza kuwasili kwenye miji ya mwambao wa jangwani kama Lüderitz na Swakopmund na kusonga mbele kwenda bara ndani.

Maafisa wa kikoloni waliiona ardhi hiyo kuwa inafaa kwa ufugaji wanyama, na muda mchache baadaye walowezi wa Kijerumani walikumbana na watu wa jamii ya Nama - na Waherero.

Vipi mahusiano yalikuwa mwanzoni?

Mwanzoni, mahusiano baina ya Wajerumani na Waherero yalikuwa mazuri, ambapo Waherero waliingia kwenye Ukristo na kukubali kuwepo kwa Wajerumani kwenye ardhi yao. Walisaini mikataba ya ulinzi na wakoloni hao ili kuwasaidia dhidi ya uvamizi wa makundi hasimu ya watu wa Nama.

Soma zaidi: Pambana! Jinsi Waafrika Mashariki walivyokabiliana na ukandamizaji wa kikoloni

Ukweli ni kuwa uvamizi ulikuwa wa pande zote mbili. Watu wa Nama na Herero walisainini mikataba ya ulinzi na Ujerumani na, matokeo yake, jamii zote mbili zikapoteza ushawishi, mifugo na ardhi yao kwa wakoloni hao.

Mambo gani yalisababisha mgogoro?

Kufikia mwaka 1903, kulikuwa na Wajerumani chini ya 5,000 waliokuwa wakiishi kwenye makoloni lakini waliokuwa wahitaji maeneo makubwa ya ardhi kwa ajili ya kilimo na ufugaji.

Serikali ya kikoloni ilifahamu hilo na ikatumia njia mbalimbali kuwapora Waherero ardhi na mifugo yao, hata kama kwa kufanya hivyo ilimaanisha kuvunja mikataba.

Soma zaidi: Kampuni ya Woermann ilivyousafirisha ukoloni wa Ujerumani

Ubaguzi wa rangi, ukosefu wa usawa mbele ya sheria baina ya wenyeji na walowezi wa Kijerumani, na kutendewa vibaya kwa watu wa Herero na Nama katika ardhi iliyomilikiwa na Wajerumani ni mambo yaliyosababisha wasiwasi kupanda hadi kiwango cha juu.

Hukumu nyepesi aliyopewa mlowezi mmoja aliyekuwa amembaka na kumuua binti wa kiongozi wa Waherero ilikuwa alama ya kiwango gani madhila hayo yalikuwa yamefikia.

Mapema mwaka 1904, wanajeshi wa Kiherero waliwauwa zaidi ya walowezi 100 wa Kijerumani.

Uasi huo - ama hatua ya kijeshi kurejesha udhibiti, kama viongozi wa Waharero walivyouona - ulisababisha hasira kubwa hadi Berlin.

Kipi kiligeuza mambo?
 

Jenerali Lothar von Trotha alichukuwa nafasi ya ukamanda wa jeshi la Wajerumani kwenye Afrika ya Kusini Magharibi katikati ya mwaka 1904 na maelfu ya wanajeshi wa Ujerumani, ama Schutztruppe, walimwagwa kwenye nchi hiyo.

Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani

02:47

This browser does not support the video element.

Sio tu kwamba von Trotha alitaka kuwashinda Waherero: Kwa maneno yake, alitaka kuwaangamiza kabisa.

Wajeshi wake waliojihami vyema kwa silaha waliwazunguka wanajeshi wa Kiherero kwenye eneo la Waterberg na kuuvunja uwezo wao wa kupambana. 


Wakati gani mapigano yaligeuka mauaji ya kimbari?


Kile kiitwacho "Amri ya Maangimizo" ilitolewa na serikali ya Ujerumani ikisema kwamba mtu yeyote wa jamii ya Herero ambaye angelionekana kwenye eneo linalomilikiwa na Ujerumani angeliuliwa.

Kivuli cha ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Kwanza

This browser does not support the audio element.

Waherero wakafukuzwa hadi kwenye jangwa kubwa la Omaheke ambalo linaungana na Botswana na lenye vyanzo vichache vya maji.

Idadi kamili haijulikani, lakini inakisiwa kuwa Waherero wapatao 80,000 - wanawake, wanaume na watoto - walikufa.

Hiyo ilikuwa ni sawa na 75% ya jamii yote kwa wakati huo - kwanza walikufa kwa kiu na njaa na kisha kutokana na utumwa wa kufanyishwa kazi kwa nguvu kwenye makambi ya mateso yaliyokuwa maeneo ya mwambao yaliyo baridi na kame katika miji ya Swakopmund na Lüderitz.

Watu wengine wa jamii ya Nama kati ya 10,000 na 20,000 waliuawa wakati wa utawala wa kikoloni. Kwa upande wao, vikosi vya Kijerumani, walipoteza chini ya wanajeshi 1,000.


Kwa nini mgogoro huu na mauaji ya kimbari bado ni habari hadi leo?


Watu wa jamii za Herero na Nama walitawanyika kote kusini mwa Afrika, na waliobakia kwenye koloni hilo la Kijerumani walilazimima kusaka kazi kwenye miji na ardhi zinazomilikiwa na Wajerumani.

Ardhi zilizoporwa ziligeuzwa mali "halali" na zikakabidhiwa ama kuuzwa kwa bei rahisi  kwa walowezi na wanajeshi wa kikoloni.

Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Pili

This browser does not support the audio element.

Miaka zaidi ya 100 baadaye, sehemu kubwa ya ardhi hizo zimo kwenye mikono ya Wanamibia wenye asili ya Kijerumani.

Tamko la pamoja lililokamilishwa mwaka 2021 liliitaka Ujerumani kutoa ahadi ya euro bilioni 1.1 (sawa na dola za Kimarekani bilioni 1.16) kwa Namibia ndani ya kipindi cha miaka 30.


Je, Ujerumani imeshalipa fidia?


Bado. Ingawa Ujerumani iliomba radhi rasmi kwa kutenda uhalifu ambao kwa mtazamo wa leo unaonekana kuwa mauaji ya kimbari, haikutambua matukio ya mwaka 1904-1908 kuwa mauaji ya kimbari kwa maana ya kisheria, jambo ambalo linamaanisha Ujerumani haiwajibiki kulipa fidia.


Viongozi wa Nama na Herero wamejibuje?


Wanasema kamwe hawakushauriwa wala hawakushirikishwa moja kwa moja kwenye mazungumzo, kwani makubaliano hayo yalikuwa baina ya serikali za Ujerumani na Namibia, sio na makundi yaliyoathirika.

Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani - Utwaaji wa ardhi

01:59

This browser does not support the video element.

Mwezi Januari 2023, wanajeshi wa jamii za Nama na Herero walijenga hoja kwamba tamko la Ujerumani na Namibia litangazwe kuwa batili kwa kupingana na vipengele kadhaa vya katiba ya Namibia. 

Mfululizo wa Makala za Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani zinatayarishwa na DW, shirika la kimataifa la utangazaji la Ujerumani kwa ufadhili wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani (AA). Ushauri wa mambo ya historia umetolewa na Profesa Lily Mafela, Profesa Kwame Osei Kwarteng na Reginald Kirey.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW