Mauaji yaendelea Syria
11 Juni 2011Matangazo
Vifo hivyo vipya vimetokea wakati wanajeshi wameanzisha operesheni ya matumizi ya nguvu ya kuzima upinzani katika mji wenye machafuko karibu na mpaka wa Uturuki.
Jana, waandamanaji walimiminika kwenye mitaa ya miji ya nchi hiyo baada ya sala ya Ijumaa, wengi wakitowa matamshi ya kejeli dhidi ya Rais Bashar al-Assad.
Wakati huo huo, katika kile kinachoonekana kama hatua kali kuwahi kuchukuliwa na Uturuki kuhusiana na machafuko hayo, Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, rafiki wa Rais Assad, ameishutumu Syria, kutokana na ghasia hizo ambazo zimesababisha zaidi ya watu 3,000 kukimbilia katika eneo la mpaka.
Mmwandishi: Grace Patricia Kabogo (AFPE,RTRE)
Mhariri: Mohamed Dahman